Safari ya Obama kwenda Kenya iko palepale.. Safari ya Miss World je?
Hali ya nchi ikiwa sio nzuri kuna vingi
vinaathirika, unaweza ukaona kwa haraka haraka tu kwamba athari kubwa ni
vifo na uharibifu wa mali za watu.. lakini ukiiangalia kiundani athari
yake ni kubbwa zaidi ya hapo.
Rolene Strauss ni mrembo wa South Africa ambaye alifanikiwa kushinda taji la Miss World 2014,
leo ndio nimejua kwamba mrembo huyu alikuwa na ratiba ziara yake
Nairobi Kenya na ilikuwa afanye hafls ya chakula cha usiku Nairobi March
10 2015 !!
Kutokana na ishu ya mashambulizi ambayo yametokea Chuo Kikuu cha Garissa Kenya, Rolene
ameahirisha safari yake na amesema yeye pamoja na timu ya watu wake
ilikuwa aje nao Kenya watatangaza tarehe nyingine ya kuja kwa ajili ya
kuja Kenya.
Kama hukujua ni kwamba mashambulizi ya Chuo hicho yamefanyika muda mfupi baada ya Rais Obama kutangaza kuwa atatembelea nchi hiyo July 2015.. hata baada ya mashambulizi kutokea bado amesema ratiba yake iko palepale.
Hutopitwa na habari yoyote inayonifikia na niko tayari kukupatia kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment