MWANANCHI
Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa
amesema kama Watanzania watashindwa kufanya mabadiliko kwa kupiga kura
kuing’oa CCM madarakani mwaka huu, hawataweza kufanya hivyo tena, huku
akihoji kama vyama tawala mbalimbali katika nchi za bara la Afrika
vimeng’oka madarakani: “Kwa nini isiwe CCM”.
Lowassa aliyeambatana na Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye
alisema vyama tawala vilivyokuwa rafiki na CCM vimeshang’oka madarakani
na kwamba hivi sasa ni zamu ya chama hicho tawala kuondolewa.
“Nataka kura nyingi ili hata
wakiiba tushinde, asilimia 90 ziwe zetu hizo 10 waache waibe.
Msipoiondoa CCM mwaka huu hatutaiondoa tena, CCM na Tanu walikuwa na
marafiki zao lakini karibu wote wameondoka.
“Chama cha Kanu cha nchini
Kenya kimeshaondoka madarakani, kile cha Malawi (Malawi Congress Party)
nacho kimeondoka, UNIP (The United National Independence Party cha
Zambia) nacho imeondoka na kile chama cha Mzee Obote (Dk Militon) cha
Uganda kimeondoka, tunaona pia jinsi Rais wa Zimbabwe (Robert
Mugabe) anavyohangaika,” Lowassa.
Katika mkutano huo, Lowassa alirudia vipaumbele vya ilani ya uchaguzi
ya Ukawa, huku akimponda mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kwa
tiketi ya CCM, Frederick Mwakalebela kuwa hawezi kushinda kwa maelezo kuwa amepanda gari bovu.
Sumaye alieleza ufisadi mbalimbali uliotokea tangu Lowassa
alipojiuzulu mwaka 2008, huku akihoji yalipo majina ya wauza dawa za
kulevya na majangili ambayo alidai kwa nyakati tofauti Rais Jakaya
Kikwete amenukuliwa akisema kuwa anayo.
Mkutano huo ulihudhuriwa na idadi kubwa ya wananchi ambao walianza
kufika uwanjani saa nne asubuhi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Baada ya kumalizika kwa mkutano huo saa 11.58 jioni, baadhi ya wananchi
hao walilisukuma gari la Lowassa na mgombea ubunge wa Iringa Mjini kwa
tiketi ya Chadema, Mchungaji Peter Msigwa hadi katikati
ya mji huo kabla ya magari hayo kushika kasi na kuwaacha wakiendelea
kukimbia barabarani huku wakiimba nyimbo mbalimbali.
Baadhi yao walionekana kubeba kitu mfano wa jeneza na kukivisha
bendera ya CCM huku wakisema mwisho wa chama hicho tawala ni Oktoba 25.
Akiwa Mafinga Mjini, Lowassa alisema anahitaji Watanzania wampigie
kura si chini ya milioni 10.2 ili awe rais na kumaliza kilio cha
wakulima nchini.
Lowassa aliwaeleza wananchi wa Mafinga kuwa amechoshwa na manyanyaso
ambayo wakulima wanaendelea kuyapata ikiwamo kukopwa mazao yao na
kutozwa ushuru na Serikali bila ya wao kupata faida yoyote.
Lowassa alisema mara atakapochaguliwa kuongoza nchi, kitu kikubwa
atakachokifanya kuwasaidia wakulima ni kufuta ushuru wote wa mazao na
kuhakikisha wananufaika na jasho wanalolitoa wakati wa kilimo.
Sumaye aliwataka wananchi wa Mafinga kutokuwa na shaka na Ukawa kwa
sababu wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi katika uchaguzi
wa Oktoba 25, licha ya CCM kujipanga kupata ushindi wa goli la mkono.
“Tunawaomba Watanzania wachague
Ukawa kwa sababu umefika muda wa mabadiliko, tunataka tupate wabunge
300, hizo nafasi nyingine wagawane vyama vingine vilivyo nje ya Ukawa,”Sumaye.
Alisema Serikali ya sasa ni dhaifu kwa sababu wamekuwa wakipeana
nafasi ya uongozi kindugu na ushikaji, hali inayofanya wananchi
kuendelea kupata shida.
Katika mkutano huo, Waziri wa zamani, Joseph Mungai alipanda jukwaani kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, William Mungai ambaye ni mwanaye.
Waziri Mungai aliyewahi kuwa mbunge kwa miaka 35 kupitia CCM na
alishika nafasi ya uwaziri katika wizara za Kilimo, Mambo ya Ndani na
Elimu, alisema wananchi wa jimbo hilo wanatakiwa kumchagua William kwa
sababu mbunge aliyemaliza muda wake hakuweza kuongoza kama alivyofanya
yeye.
Alipoulizwa baadaye kuhusu nafasi yake kisiasa, Mungai alisema tangu
aliposhtakiwa baada ya kura za maoni mwaka 2010, uanachama wake ndani ya
CCM aliuweka kando na kadi yake hajawahi kuilipia.
“Kwa hivyo mimi ni mwanasiasa mstaafu, siko katika chama chochote,” alisema.
MWANANCHI
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa
amesema amechoshwa na manyanyaso wanayoendelea kuyapata wakulima hapa
nchi kwa kukopwa mazao yao na kutozwa ushuru na serilkali bila ya wao
kupata faida yoyote.
Lowassa alisema punde atakapochaguliwa kuongaza nchi kitu kikubwa
atakachokifanya kuwasaidia wakulima ni kufuta ushuru wote wa mazao
kuhakikisha wakulima wananufaika na jasho wanalolitoa wakati wa kilimo.
Lowasa ameyasema hayo leo wilayani Mufindi alipofanya mkutano wa
hadhara wa kampeni katika Uwanja wa Shule ya Msingi Wambi, mjini
Mafinga.
Lowassa alisema watu wamekuwa wakizungumza kuwa CCM ni wezi wa kura
kwasababu ni wajanja sana katika kufanya michezo michafu katika chaguzi
na maneno hayo si yakuyabeza wala kuyafumbia macho.
“Mimi nataka kila mtu akihifazi
vizuri kichinjio chake (kadi ya kupigia kura) na siku ya kupiga kura
ikifika nawaomba wanawake na wanaume wajitokeze kwenda kupiga kura ila
wakina baba nawaomba mkishapiga kura fanyeni kazi ya kuzilinda kura
zenu” Lowassa
NIPASHE
Siku moja baada ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(UKAWA) kuzindua kampeni zake wakati wakimtambulisha mgombea urais wao, Edward Lowassa, kwa kishindo jijini Dar es Salaam, mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, ameiponda ilani yao.
Dk. Magufuli amesema CCM ndicho chama chenye ilani inayoeleweka na
imetaja mambo yanayogusa Watanzania, na siyo sawa na vyama vingine
ambvyo havina ilani na vimeshindwa kuweka vipaumbele vyao.
Akihutubia mkutano wa kampeni wilayani Ludewa, mkoa wa Njombe na Ruvuma, Dk. Magufuli alisema:
“Hadi sasa hakuna ilani ya Ukawa, leo mnawapa nchi watu ambao ni vyama vinne hadi sasa havijaweka ilani.”
Dk. Magufuli aliahidi kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Njombe
hadi Ludewa, ambayo imeshafanyiwa upembuzi yakinifu na michoro kwa
ajili ya ujenzi kuanza mwakani.
Mgombea huyo alisema serikali ya awamu ya tano itakuwa ya viwanda
kila wilaya na kwamba itaboresha huduma za umeme, majisafi na salama,
dawa mahospitalini, barabara za lami na wakulima kutokopwa mazao yao.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa jimbo la Ludewa mkoani
Njombe na Madaba wa Ruvuma, alisema pia kila kijiji kitakopeshwa Sh.
milioni 50 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vijana na wanawake zikiwa ni
jitihada za kujikwamua na umaskini.
Alisema pia serikali ya awamu ya tano itapunguza kama siyo kumaliza
kabisa kero mbalimbali katika jamii kama waendesha pikipiki maarufu kama
bodaboda kubughudhiwa na askari wa kikosi cha usalama barabarani na
mama lishe kunyang’anywa mali zao.
“Serikali yangu itakuwa ya watu wanyonge, nitahakikisha huduma muhimi
za jamii zinapatikana kwa wakati, mawaziri wangu watakuwa wa kuhudumia
wanyonge,” alisema.
Alisema alipokuwa waziri alikuwa anaagizwa, lakini kwa sasa atagiza
na akimwagiza waziri kupeleka maji sehemu fulani ni lazima afanye hivyo,
vinginevyo atafutwa kazi haraka.
Kwa mujibu wa Dk. Magufuli, kila awamu ya uongozi ina mambo yake na
kufafanua kuwa yaRais wa awamu ya kwanza, Mwalimu Julius Nyerere,
ilikuwa na kazi ya kuleta Uhuru na kuwaunganisha Watanzania na leo
wamekuwa kitu kimoja.
Alisema awamu ya pili, tatu na nne zimeliwezesha Taifa kupiga hatua
kubwa kimaendeleo na serikali yake ya awamu ya tano itakuwa ni ya
mchakamchaka wa maendeleo kwa kuwa mazingira mazuri yalitengenezwa na
watangulizi wake.
Aliahidi kuwa serikali yake itafanyakazi na vyama vyote, kwa kuwa
hakuna anayezaliwa na chama isipokuwa kinachoangaliwa ni maendeleo na
kwamba vyama si msingi wa maendeleo.
Alisema kazi kubwa itakayofanywa na serikali yake ni kuufuta umaskini na uchumi kumilikiwa na wanyonge.
NIPASHE
Mgombea udiwani wa Kata ya Bomang’ombe wilayani Hai kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Livingstone Nkya maarufu kama Ferefere, amefariki dunia ghafla muda mfupi baada ya kuzindua kampeni zake za kuwania nafasi hiyo.
Ferefere alifariki jana jioni baada ya kukimbizwa katika Hospitali ya
Rufaa ya KCMC ya mjini Moshi, kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Katibu wa CCM Wilaya ya Hai, Allan Kingazi, alilithibitishia Nipashe
kwa njia ya simu jana kuwa, mgombea huyo aliaga dunia baada ya kuzindua
kampeni za uchaguzi kwenye kata hiyo.
Alisema Ferefere alianza kuhisi afya yake inabadilika na kumfanya
kushindwa kuendelea na jukumu la kujieleza, hivyo aliamua kuondoka baada
ya mkutano huo na kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Kilimanjaro ya Mawenzi, kabla ya kuhamishiwa KCMC.
Kata ya Bomang’ombe ni miongoni mwa kata mpya tatu zilizogawanywa
katika Jimbo la Hai, lililokuwa likiwakilishwa bungeni na Mwenyekiti wa
Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.
“Ni kweli mgombea wetu
amefariki jana usiku katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC majira ya jioni;
na hivi sasa tuko kwenye taratibu za kuandaa mazishi yake. Tunasubiri
majibu ya daktari kujua amefariki dunia kutokana na tatizo gani, lakini
sisi kama CCM tutasimamisha mgombea mwingine ili kutwaa kata hiyo,” Kingazi
Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Hai, Said Mderu alipotafutwa ili
kutoa ufafanuzi iwapo uchaguzi huo utaahirishwa au laa, alisema,” Mimi sina taarifa za kifo hicho na kwa sasa nipo njiani, siwezi kuzungumza lolote. Nitafute kesho (leo) nitakuwa na majibu.
Ferefere ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu wa maduka ya vileo na
vinywaji baridi mjini hapa, alikuwa akigombea kiti hicho, akishindana na
mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joe Nkya ambaye naye ni mfanyabiashara wa maduka ya pembejeo za kilimo.
NIPASHE
Aliyewahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Chiligati,
amewapiga kijembe makada wanaohama CCM na kujiunga upinzani kuwa ni
magamba yanayojivua yenyewe na kukiacha chama hicho kikiwa kisafi na
kinachosimamia misingi yake ya kujali wakulima na wafanyakazi.
Samia Suluhu Hassan, katika Jimbo la Manyoni
Mashariki jana, Chiligati alisema CCM miaka ya nyuma iliwahi kuwataka
makada waliokuwa na kashfa mbalimbali ambayo walipewa jina la magamba
wajiondoe wenyewe na kwamba sasa ndiyo kazi hiyo imeanza kufanyika.
Chiligati ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Manyoni
Mashariki na ametangaza kustaafu siasa, alisema baada ya magamba hayo
kujivua na kumalizika, CCM kitabaki kuwa cha wafanyakazi na wakulima
kama kilivyokuwa tangu kinaasisiwa.
Alisema CCM kina wanachama zaidi ya milioni saba lakini kuna watu
wachache wanakiharibia sifa yake nzuri na kuonekana kama chama cha
mafisadi na kimetekwa na watu wenye fedha nyingi.
Samia aliahidi kwamba ikiwa chama hicho kitashinda uchaguzi mkuu
utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu, serikali yake itajenga kiwanda cha
chokaa katika jimbo hilo ili kiweze kutoa ajira kwa vijana.
Pia aliahidi ujenzi wa barabara mbalimbali, kutatua matatizo ya maji
na kulipa fidia wananchi ambao ardhi yao ilichukuliwa na serikali kwa
shughuli mbalimbali bila kulipwa.
Samia aliahidi kwamba CCM kikishinda kitaendelea kujenga minara ya
simu katika maeneo mbalimbali. Akiomba kura kwa wananchi, mgombea ubunge
wa Jimbo la Manyoni (CCM), Yahaya Masare, alisema jimbo hilo lipo nyuma
kimaendeleo lakini yeye amejipanga kutatua matatizo mbalimbali
yanayowakabili wananchi.
Alisema shida ya maji katika jimbo hilo ni kubwa na kuwaahidi wananchi kwamba atashughulikia tatizo hilo ili kulimaliza.
HABARILEO
Aliyewahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Chiligati,
amewapiga kijembe makada wanaohama CCM na kujiunga upinzani kuwa ni
magamba yanayojivua yenyewe na kukiacha chama hicho kikiwa kisafi na
kinachosimamia misingi yake ya kujali wakulima na wafanyakazi.
Samia Suluhu Hassan, katika Jimbo la Manyoni
Mashariki jana, Chiligati alisema CCM miaka ya nyuma iliwahi kuwataka
makada waliokuwa na kashfa mbalimbali ambayo walipewa jina la magamba
wajiondoe wenyewe na kwamba sasa ndiyo kazi hiyo imeanza kufanyika.
Chiligati ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Manyoni
Mashariki na ametangaza kustaafu siasa, alisema baada ya magamba hayo
kujivua na kumalizika, CCM kitabaki kuwa cha wafanyakazi na wakulima
kama kilivyokuwa tangu kinaasisiwa.
Alisema CCM kina wanachama zaidi ya milioni saba lakini kuna watu
wachache wanakiharibia sifa yake nzuri na kuonekana kama chama cha
mafisadi na kimetekwa na watu wenye fedha nyingi.
Samia aliahidi kwamba ikiwa chama hicho kitashinda uchaguzi mkuu
utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu, serikali yake itajenga kiwanda cha
chokaa katika jimbo hilo ili kiweze kutoa ajira kwa vijana.
Pia aliahidi ujenzi wa barabara mbalimbali, kutatua matatizo ya maji
na kulipa fidia wananchi ambao ardhi yao ilichukuliwa na serikali kwa
shughuli mbalimbali bila kulipwa.
Akizungumzia tatizo la mawasiliano, Samia aliahidi kwamba CCM
kikishinda kitaendelea kujenga minara ya simu katika maeneo mbalimbali.
HABARILEO
Chama cha ACT Wazalendo kimezindua kampeni zake jijini Dar es Salaam
kwa kuahidi kitakapopewa ridhaa ya kuongoza nchi, kitaunda serikali ya
Umoja wa Kitaifa.
Aidha katika uzinduzi huo ambao viongozi mbalimbali wa chama hicho walihutubia, Mgombea Urais wa chama hicho Anna Mghwira alisema wananchi wakimpa ridhaa, waziri mkuu wake atakuwa Zitto Kabwe.
“Nitakapounda serikali, katika
katiba, mtu wa kwanza kusaidiana na rais licha ya makamu, ni Zitto
Kabwe, atakuwa Waziri Mkuu katika serikali ya kwanza,” Anna Mghwira ambaye pia alisema atahusisha viongozi waadilifu kutoka CCM, Chadema na vyama vyote vya siasa na taasisi zote kiraia.
Akihutubia mkutano huo uliofanyika viwanja vya Mbagala Zakhem,
mgombea huyo, katika kuelekeza nia yake ya kuunda serikali hiyo ya
umoja, alisema linapokuja suala la kitaifa, hakuna haja ya kuangalia
masuala ya itikadi. “Mimi ni mama, hukusanya watoto wake.
Hata mama wa vifaranga hukusanya vifaranga pamoja na kuviweka kwenye
mbawa zake…mimi nina mbawa za moyo…nitaunda serikali ya umoja wa kitaifa
itakayotokana na sekta binafsi lakini kutoka watu wazalendo, wenye utu,
waadilifu, taasisi za kijamii, mashirika ya kidini, makundi ya umma ili
kuunda taswira ya nchi yetu.”
Mghwira alisema taifa linahitaji mabadiliko si ya tu kifikra na
kisera, bali pia ya kijinsia kwa kumchagua yeye kuwa Rais wa nchi.
Alisema chama chake kinatilia mkazo utu, uzalendo na uadilifu.
Makao makuu Dodoma Aidha alisema, Serikali itakapoundwa itaapishwa
Dodoma na watahakikisha wanarudisha kazi kubwa aliyoifanya Rais wa
Kwanza, Julius Nyerere ya kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi na
serikali lakini siyo makao makuu ya chama.
Alisema kuweka mji huo makao makuu, maana yake ni kuleta watu wote
kutoka pande zote za nchi. Vipaumbele Alitaja vipaumbele vyake ni kuwa
na mfumo imara na endelevu wa hifadhi ya jamii unaojengea uwezo wananchi
kukabiliana na majanga. Alisema asilimia sita pekee ya Watanzania
wanafaidika.
“Tutatumia hifadhi ya jamii kama nyenzo ya kukuza akiba nchini ili
kuwe na vyanzo vya mitaji ya uwekezaji wa ndani…tutapanua hifadhi ya
jamii kufikia makundi yote katika jamii ikiwamo wakulima, wafugaji, mama
lishe na bodaboda,” alisema. Kipaumbele kingine alichoahidi ni uchumi
shirikishi wenye kuzalisha ajira nyingi na bora.
Alisema watu wengi hawana uhakika na maisha yao kimapato. Aidha
alisema, watajikita kwenye uwekezaji wa kilimo na kusimamia uzalishaji
wake. Aidha, aliahidi kuhakikisha ardhi na mashamba yote yaliyo chini ya
mashirika ya umma, yanachukuliwa na kuwekwa chini ya uzalishaji mdogo.
Kwa upande wa viwanda, alisema atahakikisha bidhaa zinazozalishwa
nchini zinaongeza mapato ya fedha za kigeni. Chama hicho kupitia kwa
mgombea, kimesema kitaweka msukumo kwenye bidhaa za nguo na vitakuwapo
viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na mifugo.
Vipaumbele vingine ni kuhakikisha madini, mafuta na gesi, vinakuwa
mali ya wananchi kikatiba. Kuhusu Katiba Mpya, alisema wataruhusu Tume
ya Jaji Warioba imalize kazi ya katiba ilikoishia. Mgombea huyo
aliendelea kutaja vipambele vyake kuhakikisha anaboresha huduma za afya
ikiwamo kudhibiti vifo vya mama na mtoto.
Aliahidi kuondoa tatizo la watoto wa mitaani. Misamaha ya kodi kwa
mujibu wake, haitazidi asilimia moja ya pato la taifa na wakati huo huo
atadhibiti mianya ya ukwepaji kodi hususani kwa kampuni za kigeni.
Sifa za rais Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitila Mkumbo,
alishauri wananchi kuangalia wagombea urais kama wanalinda haki za
walio wengi au ni mateka wa matajiri. Mkumbo alisema, kiongozi mkuu wa
nchi, kwa maana ya rais, ana kazi kuu nne ambazo ni fikra na kutoa dira
ya nchi jambo ambalo anapaswa kuwa na uwezo wa kufikiri.
“Tatizo ni kufikiri na kutoa dira ya nchi…tunataka rais atakayetoa
misingi ya nchi, atatuletea sera..,” alisema Kitila. Alisema kazi ya
pili ya rais, ni kuwa mlinzi mkuu wa tunu za taifa huku akisisitiza
katika tunu ya umoja, wananchi kuepuka mgombea mwenye tabia za kidini,
kikabila na kikanda.
“Rais ndiye mlinzi wa usawa katika taifa…,” alisema na kushauri
wananchi kuangalia wanaogombea kama wanaelekea kulinda haki za walio
wengi au ni mateka wa matajiri. Alitaja tunu nyingine ni muungano kwa
kusema anayeomba urais na kutaka kucheza na muungano lazima akataliwe.
Kuhusu uadilifu, alisema inapaswa aingie rais atakayekoleza vita ya
ufisadi . “Kama kuna mtu anataka urais hata kutamka neno ufisadi
anaogopa, huyu hatufai hata kidogo,” alisema Kitila.
Akizungumzia demokrasia, alisema nchi imepiga hatua katika demokrasia
ambayo inahitaji rais atakayeipeleka mbele. Vile vile alisema katika
kuchagua, ni lazima kuangalia mgombea ndani ya chama chake
alipatikanaje.
“Kazi nyingine ya rais lazima awe mfano wa binadamu bora katika
jamii. Hatumaanishi malaika, tunamaanisha kwamba popote atakapoenda,
akisimama wajue huyu ni Mtanzania, awe sura ya utaifa,” alisema na
kusisitiza sifa nyingine ya rais itokane na uadilifu wa chama chake.
Kitila alisisitiza, “Mtu asiye mlaghai lazima aliyotuambia jana, na
leo yafanane. Akihubiri maji lakini yeye anakunywa wiski, yeye ni
mlaghai. Akituambia ni nyeusi jana, leo nyekundu, kesho nyeupe, huyo ni
mlaghai.” Alisisitiza kuwa ACT Wazalendo inazingatia misingi na sera
huku akibeza vyama vingine kwamba vinauza mbwembwe na ulaghai.
Ukawa wasutwa Kwa upande wake, Meneja wa Kampeni, Habib Mchange,
aliisuta Chadema na CUF kupitia viongozi wao akirejea mkutano wa Mwembe
Yanga mwaka 2007, walipotaja orodha ya waliowatuhumu kuwa mafisadi papa.
“Kipindi kile hawakuwa na Ukawa bali walikuwa na ushirikiano.
Walitaja watu wanaofilisi taifa hili ambao ni watu kumi na moja…kati
ya watu hao waliotajwa kuwa ni mafisadi, namba tisa alikuwa ni Lowassa,”
alisema Mchange. “Tulikubaliana 2007 kwamba tunapambana na CCM na wana
mafisadi. Leo naomba mtafakari…ili tusiwe wajanja wajanja lazima tuseme
ukweli.
Unayosema jana ndo hayohayo uyaseme leo,” alisema. Akinyoshea CCM pia
vidole, Mchange alilinganisha mgombea wa Ukawa sawa na chupa yenye sumu
iliyobandikwa jina la maji. Alinadi chama chake akisisitiza wananchi
wakiamini kwa kuwa kimekuja katikati ya sumu mbili za CCM na Ukawa.
Amshangaa Sumaye, Lowassa Mchange alisema anachoona ni kwamba,
ufisadi uliokuwa CCM, umezaliana na kutanuka na hatimaye kuhamia Ukawa.
“Jana (juzi) Sumaye ametulaghai… Anasema anashangaa kwa nini CCM
inaendelea kuaminiwa,” alisema.
Alikumbusha kuhusu mjadala wa kununua ndege ya rais ambayo ilipigiwa
kelele, kwamba wakati huo Sumaye ndiye alikuwa Waziri Mkuu. Pia kuhusu
ahadi ya Lowassa ya kumwachia huru mwanamuziki Nguza Viking maarufu kama
Babu Seya, Mchange alieleza kushangazwa naye kutokana na kile
alichosema, wakati anafungwa, ndiye alikuwa Waziri Mkuu.
Mchange alikuwa mkali zaidi katika hotuba yake hasa alipokuwa
anazungumzia ufisadi na wizi. “ Kumbe unaruhusiwa kuwaibia Watanzania
ukiwa CCM ukirudi upinzani ni msafi. Mwizi ni mwizi tu.
Fisadi ni fisadi tu…Wanatudanganya kwamba kuna Ukawa…waongo. Ukawa
wanatafuta rais tu. Ukawa huku chini kwa wapiga kura haupo,” alisema
Mchange. Alihoji ni namna gani mgombea urais ataweza kunadi wagombea wa
vyama vinavyounda Ukawa ambao wamegoma kuachiana majimbo hususani Jimbo
la Tabora Mjini, Serengeti na Segerea.
“Sasa tuwaulize Ukawa Lowassa akipita Tabora mjini atamnadi nani?,”
alisema akimaanisha mgombea wa CUF na Chadema wanaogombea jimbo hilo.
Zitto Kabwe Alisema ACT Wazalendo wanarejesha miiko ya uongozi.
Alisisitiza kuhusu utaratibu wa chama chake wa kiongozi kutangaza
mali na madeni yake. Zitto alisema kila chama kinachogombea, kinasema
kitapambana na rushwa na ufisadi bila kueleza ni namna gani watapambana
tofauti na ACT Wazalendo ambacho kimesema kitapambana kwa kurejesha
miiko ya uongozi.
HABARILEO
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na Mbunge wa Urambo aliyemaliza muda wake, Samuel Sitta ametaka uandaliwe mdahalo kwenye vyombo vya habari kati yake na mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa uelezwe ukweli juu ya ukweli wa sakata la Richmond.
Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge wakati Lowassa alipojiuzulu
kutokana na sakata hilo, alisema katika mdahalo huo, ataeleza ukweli juu
ya uhusika wa Lowassa katika sakata hilo na atatoa vielelezo kueleza
taifa ufisadi uliokuwa ukifanyika.
Alisema hayo jana kwenye ufunguzi wa kampeni za CCM mkoa wa Shinyanga
katika mkutano uliofanyika mjini hapa ambao wagombea wa udiwani na
ubunge wa majimbo yote ya mkoani hapa walitambulishwa.
Katika mkutano huo, alisema kujiuzulu kwa Lowassa mwaka 2008,
kulitokana na Kamati Teule iliyoongozwa na Dk Harrison Mwakyembe,
kugundua kwamba fedha za walipa kodi zilikuwa zikipotea bure.
Alisema yuko tayari kusimulia kwa umma utajiri wa mgombea huyo wa
Chadema. Makundi, urafiki Sitta ambaye ni Waziri wa Afrika Mashariki,
ambaye pia alikuwa kwenye kinyang’anyiro cha kutaka kuteuliwa kugombea
urais kupitia CCM, alisema wanamwamini Dk John Magufuli katika utendaji
wake wa kazi na pia ni kiongozi asiye na makundi au urafiki.
“Kweli lazima uwapime viongozi,
kwani anayetaka urais lazima achaguliwe kwa kufuata utaratibu,
achambuliwe usiogope moshi kama unapikia kuni…lakini mwenzetu Lowassa
hakukubaliana na hayo, akaona kaonewa kwa madai anafaa kuwa rais mbona
sisi tulikubali?,”Sitta.
Aliendelea kusema, “hali hiyo,
ilionesha ndani ya CCM kulikuwa na vyama viwili ambavyo ni ‘CCM Katiba’
na ‘CCM Maslahi’ ambayo alikuwa anaongoza Lowassa na mfuasi wake, Mgeja
(aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambaye pia alihamia
Chadema hivi karibuni).”
Wanachama mapandikizi Sitta alisema CCM ilikuwa imejaa wanachama
walio mapandikizi tofauti na sasa ambapo alidai wamekwisha jionesha na
kimekuwa chama kizuri kama ilivyokuwa enzi za hayati Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius Nyerere.
Alisisitiza kwamba kitazidi kuimarika na waliobaki wataendelea
kutetea ilani na kuhakikisha chama kinaendelea kushika dola. Kwa mujibu
wa Sitta, wakati wa mchakato, baada ya kumaliza vikao, Lowassa alikuwa
akiitisha vikao vya kundi lake alilolibatiza CCM Maslahi na kuwaagiza
wapambe wake kuitisha vyombo vya habari kushambulia watu ambao hawako
kwenye mlengo wao.
HABARILEO
Mgombea Urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia Chama Cha Demokrasia (CHADEMA) Edward Lowassa amesema kuwa endapo atafanikiwa kuwa Rais atahakikisha vituo vya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) vinakuwa vyuo vya ufundi Stadi.
Aliyasema hayo mjini Mafinga wilayani Mufindi mkoani Iringa jana
wakati wa mkutano wa kampeni kupitia umoja huo na kusema kuwa mara
vijana watakapotoka hapo watakuwa na uwezo wa kujiajiri.
Lowassa alisema kuwa kipaumbele chake kikubwa endapo atachaguliwa
atakachopigania ni pamoja na elimu mbalimbali ikiwemo ya ufundi ambayo
ni rahisi kwa kijana kupata ajira ikiwa ni pamoja na kujiajiri wao
wenyewe.
“Umefika wakati sasa kwa
kuwekeza kwenye sekta ya elimu hususani elimu ya ufundi ambayo
itawasaidia vijana kukabiliana na wimbi la ukosefu wa ajira,” alisema Lowassa.
Aidha alisema kuwa elimu itagharimiwa na serikali kuanzia sekondari
hadi chuo kikuu na anajua kuwa fedha za kuwasomesha wanafunzi kwa elimu
za sekondari na chuo kikuu zipo.
Kwa upande wake aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Frederick Sumaye alisema
kuwa lengo kubwa la Ukawa ni kuhakikisha inapata majimbo mengi ya ubunge
na udiwani ili waweze kuongoza halmashauri hapa nchini.
MTANZANIA
Mgombea urais wa Ukawa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa, amesema anahitaji kura milioni 10.2 aweze kushinda uchaguzi mkuu.
Kutokana na hali hiyo amewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi
kupiga kura Oktoba 25 mwaka huu na watakapomaliza kumpiga kura, wawe
tayari kuzilinda zisiibwe na Chama Cha Mapinduzi.
Lowassa aliyasema hayo mjini hapa jana alipohutubia maelfu ya wakazi wa Mji wa Iringa katika Uwanja wa Gangilonga.
“Mwaka huu ni lazima CCM waondoke madarakani kwa sababu vyama vikongwe vyote vyenye umri kama wa kwake vimeshaondoka.
“Angalieni Frelimo cha Msumbiji kimeshaondoka, kule Zambia nao chama
chao kimeshaondoka, kile chama cha Obote (Milton Obote Rais wa zamani wa
Uganda), kimeshaondoka, KANU cha Kenya nacho hakiko tena madarakani ila
kimebaki ZANU P F cha Zimbabwe.
“Lakini kumbeni kwamba ili nishinde nahitaji kura milioni 10.2 na
hizi zitapatikana tu kama mtajitokeza kupiga na kulinda kura zenu.
Kwa habari, matukio na ichezo ni hapahapa tangakumekuchablog