Wabunge wa upinzani Zimbabwe hawakumuacha Rais MUGABE hivi hivi…
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuzomewa na wabunge wa vyama vya upinzani wakati akilihutubia Taifa akiwa Bungeni.
Wabunge wa upinzani wa nchi hiyo walianza kuzomea wakati Mugabe akiendelea na hotuba yake jambo ambalo lilimlazimu kukaa kimya kwa muda huku wakishinikiza msimamo wao kuwa nchi hiyo haina Rais.
Awali wabunge wa upinzani walitishia kususia ufunguzi rasmi wa bunge hilo wakidai hawamtambui Rais Mugabe kama kiongozi wa Taifa hilo.
Kiongozi huyo ambaye ni mkongwe na aliyevunja rekodi ya kukaa madarakani tangu nchi hiyo ipate uhuru aliamsha hasira za wapinzani hao kwa mara nyingine baada ya kufikiwa makubaliano kuhusu kugawana madaraka ili kuumaliza mgogoro wa kisiasa uliogubika uchaguzi.
Wakati Mugabe akiwa amekaa kimya kusubiri wapinzani wanyamaze, Wabunge wa chama tawala cha ZANU PF walijibu kwa kuimba kiongozi huyo mwenye miaka 91 ataendelea kukaa madarakani.
Baada ya kutokuwepo utulivu kwa muda mrefu kiongozi huyo aliamua kusitisha hotuba yake na kuondoka.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment