Thursday, August 20, 2015

MENGI YAIBUKA BAADA YA OSCAR KUTOKA GEREZANI

Mengine kutoka Gerezani alikofungwa Oscar Pistorious… Hasira? chakula cha Sumu.. Choo na bafu? Michezo..

Jail Pisto
Toka Pistorius amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela ni October 2014, huenda yapo mengi yaliyoendelea ndani ya gereza na hukupata nafasi kuyajua… Kwa Sheria za South Africa ziko stori toka ndani ya Gereza watu wa nje wanaweza kuzipata tofauti na Sheria za nchi nyingine !!
Cha kwanza ni kwamba kumbe jamaa alikuwa mtu mwenye hasira sana siku za kwanza kwanza alivyoanza kutumikia kifungo chake, Maafisa Magereza wawili waliopata nafasi kuwa karibu nae zaidi wamesema wakati huo hakutaka hata kuongea na mtu yoyote.
oscar-pistorius-en_3079797b
Hii ilikuwa October 2014, baada ya Pistorious kuhukumiwa alipokuwa anapakiwa kwenye gari la Magereza baada ya Hukumu Mahakamani.
Siku za kwanza alikuwa anatumia mpaka saa 23 za siku nzima kukaa ndani ya chumba chake jela bila kuongea na mtu yoyote, wala kutoka nje, baadae akaanza kuzoea… >>> ‘Sasahivi ni mtu anayeweza kuongea na kucheka na mtu yoyote’—hii ni nukuu ya alichokisema Ngobeni, mmoja wa Maafisa Magereza hao.
Kingine ni kwamba kuna wakati alidai anataka kujengewa bafu lake mwenyewe kwenye chumba chake, akajengewa bafu pamoja na choo cha pekeyake.. akadai abadilishiwe kitanda, akabadilishiwa. Akataka abadilishiwe vifaa vya gym yake, navyo vikabadilishwa.
Kuna stori ambayo hii ni moja ya zilizosambaa sana mitandaoni kwamba alikuwa na hofu ya kuwekewa sumu kwenye chakula, akabadilishiwa chakula… alihitaji chakula chake kiwe kinanunuliwa kwenye Duka la Magereza.
Kgosi-Mampuru-Correctional-1022
Huu ni muonekano wa Gereza la Kgosi Mampuru II, lililopo Pretoria South Africa.
Siku chache zilizopita baada ya kuwepo kwa stori kwamba huenda akaachiwa huru na kutumikia kifungo che nje, Pistorious aliyasema haya >>> ‘Nimeikumbuka Familia yangu… natamani kuwa nao karibu zaidi, nina hamu ya kuwaona’.
Pistorious anatumikia kifungo ndani ya Gereza la Kgosi Mampuru II, Maafisa ambao wamekuwa nae karibu zaidi na kutoa stori hizo ni Violet Ngobeni na Boitumelo Morake.
.

Kwa habari, matykio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment