Tayari ninayo matokeo ya Man United Vs Club Brugge
Ikiwa zimepita siku kadhaa tu toka Ligi
Kuu mbalimbali barani Ulaya zianze August 18 imepigwa michezo kadhaa ya
kutafuta nafasi ya kufuzu kucheza katika hatua ya makundi ya Kombe la
klabu bingwa barani Ulaya, michezo iliochezwa ni pamoja na mchezo
ambao umewakutanisha Manchester United dhidi ya Club Brugge ya Ubelgiji.
Mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa nyumbani wa klabu ya Club Brugge nchini Ubelgiji katika uwanja wa Jan Breydel wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 29,472, mchezo umemalizika kwa klabu ya Manchester United kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 3-1 magoli ya Man United yakifungwa na Mephis Depay dakika ya 13 na 43 kipindi cha kwanza kabla ya goli la tatu kufungwa na Marouane Fellaini dakika ya 90 ya mchezo goli la kufutia machozi kwa klabu ya Club Brugge lilifungwa dakika ya 8 kwa Michael Carrick kujifunga.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment