MWANANCHI
Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa amesema kama Watanzania watashindwa kufanya mabadiliko kwa kupiga kura kuing’oa CCM madarakani mwaka huu, hawataweza kufanya hivyo tena, huku akihoji kama vyama tawala mbalimbali katika nchi za bara la Afrika vimeng’oka madarakani: “Kwa nini isiwe CCM”.
Lowassa aliyeambatana na Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye alisema vyama tawala vilivyokuwa rafiki na CCM vimeshang’oka madarakani na kwamba hivi sasa ni zamu ya chama hicho tawala kuondolewa.
“Nataka kura nyingi ili hata wakiiba tushinde, asilimia 90 ziwe zetu hizo 10 waache waibe. Msipoiondoa CCM mwaka huu hatutaiondoa tena, CCM na Tanu walikuwa na marafiki zao lakini karibu wote wameondoka.
“Chama cha Kanu cha nchini Kenya kimeshaondoka madarakani, kile cha Malawi (Malawi Congress Party) nacho kimeondoka, UNIP (The United National Independence Party cha Zambia) nacho imeondoka na kile chama cha Mzee Obote (Dk Militon) cha Uganda kimeondoka, tunaona pia jinsi Rais wa Zimbabwe (Robert Mugabe) anavyohangaika,” Lowassa.
Katika mkutano huo, Lowassa alirudia vipaumbele vya ilani ya uchaguzi ya Ukawa, huku akimponda mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya CCM, Frederick Mwakalebela kuwa hawezi kushinda kwa maelezo kuwa amepanda gari bovu.
Sumaye alieleza ufisadi mbalimbali uliotokea tangu Lowassa alipojiuzulu mwaka 2008, huku akihoji yalipo majina ya wauza dawa za kulevya na majangili ambayo alidai kwa nyakati tofauti Rais Jakaya Kikwete amenukuliwa akisema kuwa anayo.
Mkutano huo ulihudhuriwa na idadi kubwa ya wananchi ambao walianza kufika uwanjani saa nne asubuhi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo. Baada ya kumalizika kwa mkutano huo saa 11.58 jioni, baadhi ya wananchi hao walilisukuma gari la Lowassa na mgombea ubunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chadema, Mchungaji Peter Msigwa hadi katikati ya mji huo kabla ya magari hayo kushika kasi na kuwaacha wakiendelea kukimbia barabarani huku wakiimba nyimbo mbalimbali.
Baadhi yao walionekana kubeba kitu mfano wa jeneza na kukivisha bendera ya CCM huku wakisema mwisho wa chama hicho tawala ni Oktoba 25.
Akiwa Mafinga Mjini, Lowassa alisema anahitaji Watanzania wampigie kura si chini ya milioni 10.2 ili awe rais na kumaliza kilio cha wakulima nchini.
Lowassa aliwaeleza wananchi wa Mafinga kuwa amechoshwa na manyanyaso ambayo wakulima wanaendelea kuyapata ikiwamo kukopwa mazao yao na kutozwa ushuru na Serikali bila ya wao kupata faida yoyote.
Lowassa alisema mara atakapochaguliwa kuongoza nchi, kitu kikubwa atakachokifanya kuwasaidia wakulima ni kufuta ushuru wote wa mazao na kuhakikisha wananufaika na jasho wanalolitoa wakati wa kilimo.
Sumaye aliwataka wananchi wa Mafinga kutokuwa na shaka na Ukawa kwa sababu wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi katika uchaguzi wa Oktoba 25, licha ya CCM kujipanga kupata ushindi wa goli la mkono.
“Tunawaomba Watanzania wachague Ukawa kwa sababu umefika muda wa mabadiliko, tunataka tupate wabunge 300, hizo nafasi nyingine wagawane vyama vingine vilivyo nje ya Ukawa,”Sumaye.
Alisema Serikali ya sasa ni dhaifu kwa sababu wamekuwa wakipeana nafasi ya uongozi kindugu na ushikaji, hali inayofanya wananchi kuendelea kupata shida.
Katika mkutano huo, Waziri wa zamani, Joseph Mungai alipanda jukwaani kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, William Mungai ambaye ni mwanaye.
Waziri Mungai aliyewahi kuwa mbunge kwa miaka 35 kupitia CCM na alishika nafasi ya uwaziri katika wizara za Kilimo, Mambo ya Ndani na Elimu, alisema wananchi wa jimbo hilo wanatakiwa kumchagua William kwa sababu mbunge aliyemaliza muda wake hakuweza kuongoza kama alivyofanya yeye.
Alipoulizwa baadaye kuhusu nafasi yake kisiasa, Mungai alisema tangu aliposhtakiwa baada ya kura za maoni mwaka 2010, uanachama wake ndani ya CCM aliuweka kando na kadi yake hajawahi kuilipia.
“Kwa hivyo mimi ni mwanasiasa mstaafu, siko katika chama chochote,” alisema.
MWANANCHI
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amesema amechoshwa na manyanyaso wanayoendelea kuyapata wakulima hapa nchi kwa kukopwa mazao yao na kutozwa ushuru na serilkali bila ya wao kupata faida yoyote.
Lowassa alisema punde atakapochaguliwa kuongaza nchi kitu kikubwa atakachokifanya kuwasaidia wakulima ni kufuta ushuru wote wa mazao kuhakikisha wakulima wananufaika na jasho wanalolitoa wakati wa kilimo.
Lowasa ameyasema hayo leo wilayani Mufindi alipofanya mkutano wa hadhara wa kampeni katika Uwanja wa Shule ya Msingi Wambi, mjini Mafinga.
Lowassa alisema watu wamekuwa wakizungumza kuwa CCM ni wezi wa kura kwasababu ni wajanja sana katika kufanya michezo michafu katika chaguzi na maneno hayo si yakuyabeza wala kuyafumbia macho.
“Mimi nataka kila mtu akihifazi vizuri kichinjio chake (kadi ya kupigia kura) na siku ya kupiga kura ikifika nawaomba wanawake na wanaume wajitokeze kwenda kupiga kura ila wakina baba nawaomba mkishapiga kura fanyeni kazi ya kuzilinda kura zenu” Lowassa
NIPASHE
Siku moja baada ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kuzindua kampeni zake wakati wakimtambulisha mgombea urais wao, Edward Lowassa, kwa kishindo jijini Dar es Salaam, mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, ameiponda ilani yao.
Dk. Magufuli amesema CCM ndicho chama chenye ilani inayoeleweka na imetaja mambo yanayogusa Watanzania, na siyo sawa na vyama vingine ambvyo havina ilani na vimeshindwa kuweka vipaumbele vyao.
Akihutubia mkutano wa kampeni wilayani Ludewa, mkoa wa Njombe na Ruvuma, Dk. Magufuli alisema:
“Hadi sasa hakuna ilani ya Ukawa, leo mnawapa nchi watu ambao ni vyama vinne hadi sasa havijaweka ilani.”
Dk. Magufuli aliahidi kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Njombe hadi Ludewa, ambayo imeshafanyiwa upembuzi yakinifu na michoro kwa ajili ya ujenzi kuanza mwakani.
Mgombea huyo alisema serikali ya awamu ya tano itakuwa ya viwanda kila wilaya na kwamba itaboresha huduma za umeme, majisafi na salama, dawa mahospitalini, barabara za lami na wakulima kutokopwa mazao yao.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe na Madaba wa Ruvuma, alisema pia kila kijiji kitakopeshwa Sh. milioni 50 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vijana na wanawake zikiwa ni jitihada za kujikwamua na umaskini.
Alisema pia serikali ya awamu ya tano itapunguza kama siyo kumaliza kabisa kero mbalimbali katika jamii kama waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kubughudhiwa na askari wa kikosi cha usalama barabarani na mama lishe kunyang’anywa mali zao.
“Serikali yangu itakuwa ya watu wanyonge, nitahakikisha huduma muhimi za jamii zinapatikana kwa wakati, mawaziri wangu watakuwa wa kuhudumia wanyonge,” alisema.
Alisema alipokuwa waziri alikuwa anaagizwa, lakini kwa sasa atagiza na akimwagiza waziri kupeleka maji sehemu fulani ni lazima afanye hivyo, vinginevyo atafutwa kazi haraka.
Kwa mujibu wa Dk. Magufuli, kila awamu ya uongozi ina mambo yake na kufafanua kuwa yaRais wa awamu ya kwanza, Mwalimu Julius Nyerere, ilikuwa na kazi ya kuleta Uhuru na kuwaunganisha Watanzania na leo wamekuwa kitu kimoja.
Alisema awamu ya pili, tatu na nne zimeliwezesha Taifa kupiga hatua kubwa kimaendeleo na serikali yake ya awamu ya tano itakuwa ni ya mchakamchaka wa maendeleo kwa kuwa mazingira mazuri yalitengenezwa na watangulizi wake.
Aliahidi kuwa serikali yake itafanyakazi na vyama vyote, kwa kuwa hakuna anayezaliwa na chama isipokuwa kinachoangaliwa ni maendeleo na kwamba vyama si msingi wa maendeleo.
Alisema kazi kubwa itakayofanywa na serikali yake ni kuufuta umaskini na uchumi kumilikiwa na wanyonge.
NIPASHE
Mgombea udiwani wa Kata ya Bomang’ombe wilayani Hai kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Livingstone Nkya maarufu kama Ferefere, amefariki dunia ghafla muda mfupi baada ya kuzindua kampeni zake za kuwania nafasi hiyo.
Ferefere alifariki jana jioni baada ya kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya mjini Moshi, kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Katibu wa CCM Wilaya ya Hai, Allan Kingazi, alilithibitishia Nipashe kwa njia ya simu jana kuwa, mgombea huyo aliaga dunia baada ya kuzindua kampeni za uchaguzi kwenye kata hiyo.
Alisema Ferefere alianza kuhisi afya yake inabadilika na kumfanya kushindwa kuendelea na jukumu la kujieleza, hivyo aliamua kuondoka baada ya mkutano huo na kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi, kabla ya kuhamishiwa KCMC.
Kata ya Bomang’ombe ni miongoni mwa kata mpya tatu zilizogawanywa katika Jimbo la Hai, lililokuwa likiwakilishwa bungeni na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.
“Ni kweli mgombea wetu amefariki jana usiku katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC majira ya jioni; na hivi sasa tuko kwenye taratibu za kuandaa mazishi yake. Tunasubiri majibu ya daktari kujua amefariki dunia kutokana na tatizo gani, lakini sisi kama CCM tutasimamisha mgombea mwingine ili kutwaa kata hiyo,” Kingazi
Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Hai, Said Mderu alipotafutwa ili kutoa ufafanuzi iwapo uchaguzi huo utaahirishwa au laa, alisema,” Mimi sina taarifa za kifo hicho na kwa sasa nipo njiani, siwezi kuzungumza lolote. Nitafute kesho (leo) nitakuwa na majibu.
Ferefere ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu wa maduka ya vileo na vinywaji baridi mjini hapa, alikuwa akigombea kiti hicho, akishindana na mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joe Nkya ambaye naye ni mfanyabiashara wa maduka ya pembejeo za kilimo.
NIPASHE
Aliyewahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Chiligati, amewapiga kijembe makada wanaohama CCM na kujiunga upinzani kuwa ni magamba yanayojivua yenyewe na kukiacha chama hicho kikiwa kisafi na kinachosimamia misingi yake ya kujali wakulima na wafanyakazi.
Samia Suluhu Hassan, katika Jimbo la Manyoni Mashariki jana, Chiligati alisema CCM miaka ya nyuma iliwahi kuwataka makada waliokuwa na kashfa mbalimbali ambayo walipewa jina la magamba wajiondoe wenyewe na kwamba sasa ndiyo kazi hiyo imeanza kufanyika.
Chiligati ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki na ametangaza kustaafu siasa, alisema baada ya magamba hayo kujivua na kumalizika, CCM kitabaki kuwa cha wafanyakazi na wakulima kama kilivyokuwa tangu kinaasisiwa.
Alisema CCM kina wanachama zaidi ya milioni saba lakini kuna watu wachache wanakiharibia sifa yake nzuri na kuonekana kama chama cha mafisadi na kimetekwa na watu wenye fedha nyingi.
Samia aliahidi kwamba ikiwa chama hicho kitashinda uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu, serikali yake itajenga kiwanda cha chokaa katika jimbo hilo ili kiweze kutoa ajira kwa vijana.
Pia aliahidi ujenzi wa barabara mbalimbali, kutatua matatizo ya maji na kulipa fidia wananchi ambao ardhi yao ilichukuliwa na serikali kwa shughuli mbalimbali bila kulipwa.
Samia aliahidi kwamba CCM kikishinda kitaendelea kujenga minara ya simu katika maeneo mbalimbali. Akiomba kura kwa wananchi, mgombea ubunge wa Jimbo la Manyoni (CCM), Yahaya Masare, alisema jimbo hilo lipo nyuma kimaendeleo lakini yeye amejipanga kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili wananchi.
Alisema shida ya maji katika jimbo hilo ni kubwa na kuwaahidi wananchi kwamba atashughulikia tatizo hilo ili kulimaliza.
HABARILEO
Aliyewahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Chiligati, amewapiga kijembe makada wanaohama CCM na kujiunga upinzani kuwa ni magamba yanayojivua yenyewe na kukiacha chama hicho kikiwa kisafi na kinachosimamia misingi yake ya kujali wakulima na wafanyakazi.
Samia Suluhu Hassan, katika Jimbo la Manyoni Mashariki jana, Chiligati alisema CCM miaka ya nyuma iliwahi kuwataka makada waliokuwa na kashfa mbalimbali ambayo walipewa jina la magamba wajiondoe wenyewe na kwamba sasa ndiyo kazi hiyo imeanza kufanyika.
Chiligati ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki na ametangaza kustaafu siasa, alisema baada ya magamba hayo kujivua na kumalizika, CCM kitabaki kuwa cha wafanyakazi na wakulima kama kilivyokuwa tangu kinaasisiwa.
Alisema CCM kina wanachama zaidi ya milioni saba lakini kuna watu wachache wanakiharibia sifa yake nzuri na kuonekana kama chama cha mafisadi na kimetekwa na watu wenye fedha nyingi.
Samia aliahidi kwamba ikiwa chama hicho kitashinda uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu, serikali yake itajenga kiwanda cha chokaa katika jimbo hilo ili kiweze kutoa ajira kwa vijana.
Pia aliahidi ujenzi wa barabara mbalimbali, kutatua matatizo ya maji na kulipa fidia wananchi ambao ardhi yao ilichukuliwa na serikali kwa shughuli mbalimbali bila kulipwa.
Akizungumzia tatizo la mawasiliano, Samia aliahidi kwamba CCM kikishinda kitaendelea kujenga minara ya simu katika maeneo mbalimbali.
HABARILEO
Chama cha ACT Wazalendo kimezindua kampeni zake jijini Dar es Salaam kwa kuahidi kitakapopewa ridhaa ya kuongoza nchi, kitaunda serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Aidha katika uzinduzi huo ambao viongozi mbalimbali wa chama hicho walihutubia, Mgombea Urais wa chama hicho Anna Mghwira alisema wananchi wakimpa ridhaa, waziri mkuu wake atakuwa Zitto Kabwe.
“Nitakapounda serikali, katika katiba, mtu wa kwanza kusaidiana na rais licha ya makamu, ni Zitto Kabwe, atakuwa Waziri Mkuu katika serikali ya kwanza,” Anna Mghwira ambaye pia alisema atahusisha viongozi waadilifu kutoka CCM, Chadema na vyama vyote vya siasa na taasisi zote kiraia.
Akihutubia mkutano huo uliofanyika viwanja vya Mbagala Zakhem, mgombea huyo, katika kuelekeza nia yake ya kuunda serikali hiyo ya umoja, alisema linapokuja suala la kitaifa, hakuna haja ya kuangalia masuala ya itikadi. “Mimi ni mama, hukusanya watoto wake.
Hata mama wa vifaranga hukusanya vifaranga pamoja na kuviweka kwenye mbawa zake…mimi nina mbawa za moyo…nitaunda serikali ya umoja wa kitaifa itakayotokana na sekta binafsi lakini kutoka watu wazalendo, wenye utu, waadilifu, taasisi za kijamii, mashirika ya kidini, makundi ya umma ili kuunda taswira ya nchi yetu.”
Mghwira alisema taifa linahitaji mabadiliko si ya tu kifikra na kisera, bali pia ya kijinsia kwa kumchagua yeye kuwa Rais wa nchi. Alisema chama chake kinatilia mkazo utu, uzalendo na uadilifu.
Makao makuu Dodoma Aidha alisema, Serikali itakapoundwa itaapishwa Dodoma na watahakikisha wanarudisha kazi kubwa aliyoifanya Rais wa Kwanza, Julius Nyerere ya kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi na serikali lakini siyo makao makuu ya chama.
Alisema kuweka mji huo makao makuu, maana yake ni kuleta watu wote kutoka pande zote za nchi. Vipaumbele Alitaja vipaumbele vyake ni kuwa na mfumo imara na endelevu wa hifadhi ya jamii unaojengea uwezo wananchi kukabiliana na majanga. Alisema asilimia sita pekee ya Watanzania wanafaidika.
“Tutatumia hifadhi ya jamii kama nyenzo ya kukuza akiba nchini ili kuwe na vyanzo vya mitaji ya uwekezaji wa ndani…tutapanua hifadhi ya jamii kufikia makundi yote katika jamii ikiwamo wakulima, wafugaji, mama lishe na bodaboda,” alisema. Kipaumbele kingine alichoahidi ni uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira nyingi na bora.
Alisema watu wengi hawana uhakika na maisha yao kimapato. Aidha alisema, watajikita kwenye uwekezaji wa kilimo na kusimamia uzalishaji wake. Aidha, aliahidi kuhakikisha ardhi na mashamba yote yaliyo chini ya mashirika ya umma, yanachukuliwa na kuwekwa chini ya uzalishaji mdogo.
Kwa upande wa viwanda, alisema atahakikisha bidhaa zinazozalishwa nchini zinaongeza mapato ya fedha za kigeni. Chama hicho kupitia kwa mgombea, kimesema kitaweka msukumo kwenye bidhaa za nguo na vitakuwapo viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na mifugo.
Vipaumbele vingine ni kuhakikisha madini, mafuta na gesi, vinakuwa mali ya wananchi kikatiba. Kuhusu Katiba Mpya, alisema wataruhusu Tume ya Jaji Warioba imalize kazi ya katiba ilikoishia. Mgombea huyo aliendelea kutaja vipambele vyake kuhakikisha anaboresha huduma za afya ikiwamo kudhibiti vifo vya mama na mtoto.
Aliahidi kuondoa tatizo la watoto wa mitaani. Misamaha ya kodi kwa mujibu wake, haitazidi asilimia moja ya pato la taifa na wakati huo huo atadhibiti mianya ya ukwepaji kodi hususani kwa kampuni za kigeni.
Sifa za rais Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitila Mkumbo, alishauri wananchi kuangalia wagombea urais kama wanalinda haki za walio wengi au ni mateka wa matajiri. Mkumbo alisema, kiongozi mkuu wa nchi, kwa maana ya rais, ana kazi kuu nne ambazo ni fikra na kutoa dira ya nchi jambo ambalo anapaswa kuwa na uwezo wa kufikiri.
“Tatizo ni kufikiri na kutoa dira ya nchi…tunataka rais atakayetoa misingi ya nchi, atatuletea sera..,” alisema Kitila. Alisema kazi ya pili ya rais, ni kuwa mlinzi mkuu wa tunu za taifa huku akisisitiza katika tunu ya umoja, wananchi kuepuka mgombea mwenye tabia za kidini, kikabila na kikanda.
“Rais ndiye mlinzi wa usawa katika taifa…,” alisema na kushauri wananchi kuangalia wanaogombea kama wanaelekea kulinda haki za walio wengi au ni mateka wa matajiri. Alitaja tunu nyingine ni muungano kwa kusema anayeomba urais na kutaka kucheza na muungano lazima akataliwe.
Kuhusu uadilifu, alisema inapaswa aingie rais atakayekoleza vita ya ufisadi . “Kama kuna mtu anataka urais hata kutamka neno ufisadi anaogopa, huyu hatufai hata kidogo,” alisema Kitila.
Akizungumzia demokrasia, alisema nchi imepiga hatua katika demokrasia ambayo inahitaji rais atakayeipeleka mbele. Vile vile alisema katika kuchagua, ni lazima kuangalia mgombea ndani ya chama chake alipatikanaje.
“Kazi nyingine ya rais lazima awe mfano wa binadamu bora katika jamii. Hatumaanishi malaika, tunamaanisha kwamba popote atakapoenda, akisimama wajue huyu ni Mtanzania, awe sura ya utaifa,” alisema na kusisitiza sifa nyingine ya rais itokane na uadilifu wa chama chake.
Kitila alisisitiza, “Mtu asiye mlaghai lazima aliyotuambia jana, na leo yafanane. Akihubiri maji lakini yeye anakunywa wiski, yeye ni mlaghai. Akituambia ni nyeusi jana, leo nyekundu, kesho nyeupe, huyo ni mlaghai.” Alisisitiza kuwa ACT Wazalendo inazingatia misingi na sera huku akibeza vyama vingine kwamba vinauza mbwembwe na ulaghai.
Ukawa wasutwa Kwa upande wake, Meneja wa Kampeni, Habib Mchange, aliisuta Chadema na CUF kupitia viongozi wao akirejea mkutano wa Mwembe Yanga mwaka 2007, walipotaja orodha ya waliowatuhumu kuwa mafisadi papa. “Kipindi kile hawakuwa na Ukawa bali walikuwa na ushirikiano.
Walitaja watu wanaofilisi taifa hili ambao ni watu kumi na moja…kati ya watu hao waliotajwa kuwa ni mafisadi, namba tisa alikuwa ni Lowassa,” alisema Mchange. “Tulikubaliana 2007 kwamba tunapambana na CCM na wana mafisadi. Leo naomba mtafakari…ili tusiwe wajanja wajanja lazima tuseme ukweli.
Unayosema jana ndo hayohayo uyaseme leo,” alisema. Akinyoshea CCM pia vidole, Mchange alilinganisha mgombea wa Ukawa sawa na chupa yenye sumu iliyobandikwa jina la maji. Alinadi chama chake akisisitiza wananchi wakiamini kwa kuwa kimekuja katikati ya sumu mbili za CCM na Ukawa.
Amshangaa Sumaye, Lowassa Mchange alisema anachoona ni kwamba, ufisadi uliokuwa CCM, umezaliana na kutanuka na hatimaye kuhamia Ukawa. “Jana (juzi) Sumaye ametulaghai… Anasema anashangaa kwa nini CCM inaendelea kuaminiwa,” alisema.
Alikumbusha kuhusu mjadala wa kununua ndege ya rais ambayo ilipigiwa kelele, kwamba wakati huo Sumaye ndiye alikuwa Waziri Mkuu. Pia kuhusu ahadi ya Lowassa ya kumwachia huru mwanamuziki Nguza Viking maarufu kama Babu Seya, Mchange alieleza kushangazwa naye kutokana na kile alichosema, wakati anafungwa, ndiye alikuwa Waziri Mkuu.
Mchange alikuwa mkali zaidi katika hotuba yake hasa alipokuwa anazungumzia ufisadi na wizi. “ Kumbe unaruhusiwa kuwaibia Watanzania ukiwa CCM ukirudi upinzani ni msafi. Mwizi ni mwizi tu.
Fisadi ni fisadi tu…Wanatudanganya kwamba kuna Ukawa…waongo. Ukawa wanatafuta rais tu. Ukawa huku chini kwa wapiga kura haupo,” alisema Mchange. Alihoji ni namna gani mgombea urais ataweza kunadi wagombea wa vyama vinavyounda Ukawa ambao wamegoma kuachiana majimbo hususani Jimbo la Tabora Mjini, Serengeti na Segerea.
“Sasa tuwaulize Ukawa Lowassa akipita Tabora mjini atamnadi nani?,” alisema akimaanisha mgombea wa CUF na Chadema wanaogombea jimbo hilo. Zitto Kabwe Alisema ACT Wazalendo wanarejesha miiko ya uongozi.
Alisisitiza kuhusu utaratibu wa chama chake wa kiongozi kutangaza mali na madeni yake. Zitto alisema kila chama kinachogombea, kinasema kitapambana na rushwa na ufisadi bila kueleza ni namna gani watapambana tofauti na ACT Wazalendo ambacho kimesema kitapambana kwa kurejesha miiko ya uongozi.
HABARILEO
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na Mbunge wa Urambo aliyemaliza muda wake, Samuel Sitta ametaka uandaliwe mdahalo kwenye vyombo vya habari kati yake na mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa uelezwe ukweli juu ya ukweli wa sakata la Richmond.
Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge wakati Lowassa alipojiuzulu kutokana na sakata hilo, alisema katika mdahalo huo, ataeleza ukweli juu ya uhusika wa Lowassa katika sakata hilo na atatoa vielelezo kueleza taifa ufisadi uliokuwa ukifanyika.
Alisema hayo jana kwenye ufunguzi wa kampeni za CCM mkoa wa Shinyanga katika mkutano uliofanyika mjini hapa ambao wagombea wa udiwani na ubunge wa majimbo yote ya mkoani hapa walitambulishwa.
Katika mkutano huo, alisema kujiuzulu kwa Lowassa mwaka 2008, kulitokana na Kamati Teule iliyoongozwa na Dk Harrison Mwakyembe, kugundua kwamba fedha za walipa kodi zilikuwa zikipotea bure.
Alisema yuko tayari kusimulia kwa umma utajiri wa mgombea huyo wa Chadema. Makundi, urafiki Sitta ambaye ni Waziri wa Afrika Mashariki, ambaye pia alikuwa kwenye kinyang’anyiro cha kutaka kuteuliwa kugombea urais kupitia CCM, alisema wanamwamini Dk John Magufuli katika utendaji wake wa kazi na pia ni kiongozi asiye na makundi au urafiki.
“Kweli lazima uwapime viongozi, kwani anayetaka urais lazima achaguliwe kwa kufuata utaratibu, achambuliwe usiogope moshi kama unapikia kuni…lakini mwenzetu Lowassa hakukubaliana na hayo, akaona kaonewa kwa madai anafaa kuwa rais mbona sisi tulikubali?,”Sitta.
Aliendelea kusema, “hali hiyo, ilionesha ndani ya CCM kulikuwa na vyama viwili ambavyo ni ‘CCM Katiba’ na ‘CCM Maslahi’ ambayo alikuwa anaongoza Lowassa na mfuasi wake, Mgeja (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambaye pia alihamia Chadema hivi karibuni).”
Wanachama mapandikizi Sitta alisema CCM ilikuwa imejaa wanachama walio mapandikizi tofauti na sasa ambapo alidai wamekwisha jionesha na kimekuwa chama kizuri kama ilivyokuwa enzi za hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Alisisitiza kwamba kitazidi kuimarika na waliobaki wataendelea kutetea ilani na kuhakikisha chama kinaendelea kushika dola. Kwa mujibu wa Sitta, wakati wa mchakato, baada ya kumaliza vikao, Lowassa alikuwa akiitisha vikao vya kundi lake alilolibatiza CCM Maslahi na kuwaagiza wapambe wake kuitisha vyombo vya habari kushambulia watu ambao hawako kwenye mlengo wao.
HABARILEO
Mgombea Urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia Chama Cha Demokrasia (CHADEMA) Edward Lowassa amesema kuwa endapo atafanikiwa kuwa Rais atahakikisha vituo vya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) vinakuwa vyuo vya ufundi Stadi.
Aliyasema hayo mjini Mafinga wilayani Mufindi mkoani Iringa jana wakati wa mkutano wa kampeni kupitia umoja huo na kusema kuwa mara vijana watakapotoka hapo watakuwa na uwezo wa kujiajiri.
Lowassa alisema kuwa kipaumbele chake kikubwa endapo atachaguliwa atakachopigania ni pamoja na elimu mbalimbali ikiwemo ya ufundi ambayo ni rahisi kwa kijana kupata ajira ikiwa ni pamoja na kujiajiri wao wenyewe.
“Umefika wakati sasa kwa kuwekeza kwenye sekta ya elimu hususani elimu ya ufundi ambayo itawasaidia vijana kukabiliana na wimbi la ukosefu wa ajira,” alisema Lowassa.
Aidha alisema kuwa elimu itagharimiwa na serikali kuanzia sekondari hadi chuo kikuu na anajua kuwa fedha za kuwasomesha wanafunzi kwa elimu za sekondari na chuo kikuu zipo.
Kwa upande wake aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Frederick Sumaye alisema kuwa lengo kubwa la Ukawa ni kuhakikisha inapata majimbo mengi ya ubunge na udiwani ili waweze kuongoza halmashauri hapa nchini.
MTANZANIA
Mgombea urais wa Ukawa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa, amesema anahitaji kura milioni 10.2 aweze kushinda uchaguzi mkuu.
Kutokana na hali hiyo amewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kupiga kura Oktoba 25 mwaka huu na watakapomaliza kumpiga kura, wawe tayari kuzilinda zisiibwe na Chama Cha Mapinduzi.
Lowassa aliyasema hayo mjini hapa jana alipohutubia maelfu ya wakazi wa Mji wa Iringa katika Uwanja wa Gangilonga.
“Mwaka huu ni lazima CCM waondoke madarakani kwa sababu vyama vikongwe vyote vyenye umri kama wa kwake vimeshaondoka.
“Angalieni Frelimo cha Msumbiji kimeshaondoka, kule Zambia nao chama chao kimeshaondoka, kile chama cha Obote (Milton Obote Rais wa zamani wa Uganda), kimeshaondoka, KANU cha Kenya nacho hakiko tena madarakani ila kimebaki ZANU P F cha Zimbabwe.
“Lakini kumbeni kwamba ili nishinde nahitaji kura milioni 10.2 na hizi zitapatikana tu kama mtajitokeza kupiga na kulinda kura zenu.
Kwa habari, matukio na ichezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment