Tuesday, August 18, 2015

ARSENAL KUMKOSA BENZEMA

Arsenal yamkosa Benzema.


French national soccer team player Karim Benzema (L) signs autographs as he arrives at a news conference to sign his exclusive renewal contract with sporting goods maker Adidas in Paris May 22, 2012.  REUTERS/Gonzalo Fuentes  (FRANCE - Tags: SPORT SOCCER BUSINESS)

Huku kukiwa na matumaini miongoni mwa mashabiki wa Arsenal juu ya uwezekano wa kumsajili mshambuliaji raia wa Ufaransa Karim Benzema , kocha wa Real Madrid Rafael Benitez amethibitisha kuwa mshambuliaji huyo hatauzwa kama ilivyodaiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari.
Benitez amesema kuwa mshambuliaji huyo ni sehemu kubwa ya mipango yake  msimu huu na kwa sababu hiyo hategemei kuona akiondoka na kuhamia klabu nyingine kama inavyoandikwa magazetini.
Karim Benzema ametajwa kuwa sehemu ya mpango wa mkakati wa usajili ndani ya klabu ya Arsenal huku kocha Arsene Wenger akitengenewa kiasi kikubwa cha fedha ili aweze kumsajili mchezaji huyo .
Hivi karibuni zilizuka habari kuwa Bodi ya klabu hiyo yenye maskani yake maeneo ya kusini mwa London imetoa idhini kwa Wenger kufanya jaribio la kumsajili Benzema jaribio ambalo halijafanikiwa .
Hadi sasa Arsenal inamtegemea zaidi Olivier Giroud kama mshambuliaji wake kinara huku Danny Welbeck akiwa majeruhi hali ambayo imelazimu klabu hii kuingia sokoni kusaka mshambuliaji nyota.

No comments:

Post a Comment