Saturday, August 22, 2015

MUUNGANISHO WA WAJASIRIAMALI (MUVI) TANGA WAWAWEZESHA WAJASIRIAMALI WILAYA NNE TANGA



Tangakumekuchablog
Tanga, WAJASIRIAMALI kilimo cha Machungwa na Maharage Tanga wamelalamikia ukosefu wa masoko ya kuuzia bidhaa zao na badala yake wamekuwa wakilanguliwa na matajiri kwa kuwauzia bei ya kutupa.
Wakizungumza wakati wa kilele cha kufunga mafunzo ya Ujasiriamali yaliyoandaliwa na Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana , walisema wanashindwa kukiendeleza kilimo chao kutokana na kutokuwepo kwa soko la uhakika.
Walisema kilimo hicho kama Serikali haitojenga kiwanda cha kusindika matunda kinaweza kutoweka na wakulima kubadilisha aina ya kilimo na ramani ya zao la machungwa na maharage Tanga kutoweka.
‘Tunaiomba Serikali kukiokoa kilimo cha machungwa na maharage kwa kutuwekea soko la uhakika-----kipindi cha mavuno watu wenye pesa huzuka na kututisha kuporomoka kwa soko” alisema Josephene Kapinga na kuongeza
“Kutokana na uelewa wetu mdogo wa masoko  tunakubali na mwisho wa mavuno ukipiga hesabu ni hasara tupu-----tunaiomba Serikali kutuangalia vyenginevyo tutakuwa watumwa wa matajiri” alisema
Akifunga mafunzo hayo, Meneja wa Sido Tanga, Rubben Gurumo, amevitaka vikundi vya Ujasiriamali kuimarisha umoja wao ili kuweza kupata fursa za mikopo kwnye taasisi za fedha na Mabenki.
Alisema kuna vikundi vingi vya ujaririsamali zikiwemo za kazi za mikono hufa kutokana na kutokuwa na umoja wa kweli na hivyo huishia njiani jambo ambalo hukosa fursa nyingi za kujikomboa kimaendeleo.
“Kuna vikundi vingi huanza kwa kasi ila baadae huishia njiani na kufa kabisa----hii ni kutokana na kutokuwa na uongozi imara na kujiwekea katiba ambayo itawaongoza ikiwa lengo ni kuyafikia malengo waliyojiwekea.” Alisema Gurumo
Alisema ili kuweza vikundi hivyo kuwa endelevu na vyenye tija na kuwakomboa ni wajibu wa kutafuta masoko ya ndani na nje na kuweza kuuza bidhaa zao jambo ambalo litwatangaza  kitaifa na kimataifa.
                                          Mwisho







 ,Wajasiriamali wanawake kutoka Wilayani Korogwe Mkoani Tanga, wakifunga unga katika paketi mara baada ya kuhitimu mafunzo ya siku sita  yaliyoendeshwa na Muunganisho wa Wajasiriamali Vijijini (MUVI) jana Tanga ambapo jumla ya wahitimu 31 waliweza kuhitimu mafunzo yao.














 Wahitimu wa mafunzo ya Ujasiriamali kutoka Wilaya za Kilindi, Handeni, Korogwe na Pangani, wakisikiliza hutuba ya mgeni rasmi mara baada ya kutunukiwa vyeti vyao baada ya kuhitimu mafunzo ya Ujasiriamali yaliyoendeshwa kwa siku sita na Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI) na kufikia kilele chake  jana ambapo jumla ya wahitim 31 waliweza  kuhitimu mafunzo yao.

  Meneja wa Sido Mkoani Tanga, Rubben Gurumo, akizungumza wahitimu wa mafunzo ya Ujasiriamali kutoka Wilaya za Kilindi, Handeni, Korogwe na Pangani mafunzo yaliyoendeshwa kwa siku sita na Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI), (kushoto) ni Afisa Maendeleo Biashara wa Sido Tanga, Gladyness Foya (kulia) ni Katibu wa kikundi cha Marejo Group cha Korogwe,Maria Emmanuel . Jumla ya watimu 31 waliweza kuhitimu mafunzo yao

 Meneja wa Sido Tanga, Rubben Gurumo akizungumza na Wajasiriamali kutoka Wilaya za Kilindi, Handeni, Korogwe na Pangani mara baada kuhitimu mafunzo ya siku sita yaliyoendeshwa na Muunganisho wa Wajasiriamali Vijijini (MUVI) na kuendeshwa kwa siku sita ambapo jumla ya wahitimi 31 waliweza kuhitimu mafunzo yao jana.

 Wajasiriamali kutoka Wilaya za Kilindi , Handeni, Korogwe, Muheza na Pangani wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa na vyeti vyao na mgeni rasmi mara baada ya kupatiwa vyeti vyao na kufanyika hafla fupi

No comments:

Post a Comment