Wakazi wa mtaa wa Majengo mapya Kwaminchi Tanga wakipita katika barabara
iliyozagaa takataka na kuwa kero kwa wakazi wa eneo hilo na kusababisha wadudu
wachafu kuingia katika makazi ya watu na usumbufu
kwa wapita njia.
Imekuwa ada kwa watu mitaani kujitupia takataka ovyo bila kuzingatia mazingira na Afya za wakazi wa maeneo husika.
Hii imekuwa kero kwa wakazi wa maeneo hayo na wapita njia huku mamlaka zinazohusika kusimamia usafi zikiwa zimekaa kimya na kuibuka wakati wa matatizo hasa magonjwa ya miripuko (Kipindupindu)
Katika jiji la Tanga mbali ya halmashauri ya jiji kufanya jitihada za kuhakikisha jiji hilo linakuwa katika mazingira ya usafi , lakini inadaiwa sheria zake ambazo imejiwekea zimekuwa hazifuatwi na hivyo kuwa kero.
Baadhi ya maeneo hsa katika masoko uchafu unadaiwa kukithiri mbali ya mitaani ambako kumezoeleka ndiko hasa hakufai.
Mitaa ambayo inadaiwa kuongoza kwa uchafu ni, Makorora, Kwaminchi, Mikanjuni, Mabawa na Mwahako.
Ningefurhi kupata maoni yako eneo ambalo unaishi hali ikoje, ungana nami hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment