Wednesday, August 19, 2015

OSCAR PISTORIUS KUTUMIKIA KIFUNGO CHA NJE

Oscar Pistorious anarudi uraiani? Jela kuna VIP? haya hapa kutoka South Africa..

oscar-pistorius-600
Oscar Pistorious wakati kesi yake inaendelea Mahakamani Afrika Kusini.
Mwezi October 2014 iliytolewa hukumu ya kifungo cha miaka mitano jela kwa kesi ya mauaji ambayo ilikuwa inamkabili Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorious.
Stori nyingine iliyopewa uzito sasahivi inahusu ishu ya Mwanariadha huyo kuachiwa kutoka gerezani Ijumaa ya wiki hii August 21 2015 na kutumikia Kifungo cha nje, huku akiwa na jukumu la kuripoti Kituo cha Polisi kila siku.
Oscar Pistorious alikuwa na kesi ya mauaji kutokana na tukio la kumpiga risasi aliyekuwa mpenzi wake, Reeva Steenkamp ndani ya nyumba yake.
Oscar
Picha ya zamani kabla ya Reeva Steenkamp hajafariki, hapo alikuwa na mpenzi wake Oscar Pistorious.
Ripoti ya kuachiwa kwa Pistorious inakuja baada ya jamaa huyo kuwa tayari ametumikia miezi 10 jela tangu ahukumiwe na Mahakama Kuu ya South Africa.
Pistorious atakuwa kwenye kifungo kwenye Jumba la Kifahari la mjomba wake huku akiwa na kifaa maalum mguuni ambacho hatotakiwa kukivua hata mara moja, na mwenendo wake utakuwa ukifuatiliwa wakati wote na watu wa usalama kupitia kifaa hicho.
Uhuru mwingine ambao atakuwa nao ni wa kwenda mahali popote kwa ajili ya shughuli muhimu pamoja na kukutana na ndugu zake.
pistorius_2127920a
Japo inaonekana kifungo chake kinaendelea kupata nafuu zaidi bado Wanasheria wanashughulika na kuhakikisha Rufaa ya Kesi yake inasikilizwa ili kumlegezea adhabu ya kifungo cha miaka mitano jela.
Stori nyingine toka jela zinaonesha jamaa anaishi maisha tofauti na wafungwa wengine >>> “Pistorious alikuwa ni VIP gerezani”—haya ni maneno ya mfungwa mmoja, Boswell Mhlongo ambaye walikuwa gereza moja la Kgosi Mapuru II, Pretoria.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapaha tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment