Saturday, August 22, 2015

SUMAYE NAE ATIMKIA UKAWA

 Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye nae atimkia  UKAWA..

UKAWA II
Stori za Siasa na uzito wake, zinatufikia mpya kila siku na kila mpya inayonifikia na mimi nakusogezea… hii imenifikia dakika chache zilizopita kutoka Bahari Beach Dar es Salaam, Ukumbi uleule ambao July 28 2015 Mbunge wa Monduli anayemaliza muda wake na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa alitangaza kujiunga CHADEMA, leo Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Tluway Sumaye naye ametangaza kujiunga na Umoja wa Vyama vya UKAWA.
MMGL0986
Mawaziri Wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye.
Frederick Tluway Sumaye ametumikia miaka kumi kwenye nafasi ya Uwaziri Mkuu wakati Mzee Benjamin William Mkapa akiwa Rais wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 mpaka 2005… kwenye nilichomnukuu wakati akitangaza uamuzi huo kuna hizi sentensi pia.
Mzee Sumaye ni mmoja wa Makada wa CCM waliochukua Fomu kuwania kupituishwa kwenye nafai ya Urais CCM lakini hakufaniukiwa kushinda nafasi hiyo
Mzee Sumaye ni mmoja wa Makada wa CCM waliochukua Fomu kuwania kupitishwa kwenye nafasi ya Urais CCM lakini hakufanikiwa kupita kwenye nafasi hiyo.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment