Hizi ni kauli tatu za Balotelli kuhusu Liverpool na masharti aliyopewa AC Milan
Mshambuliaji wa kimataifa wa Italia Mario Balotelli
ambaye huwa ni kawaida kuwa katika headlines mbalimbali kutokana na
tabia yake na matukio yake ambayo anafanya, August 27 kaongea sababu
zilizomfanya asifanye vizuri akiwa Liverpool.
Balotelli alikuwa na maisha magumu Liverpool kwani msimu uliomalizika aliishia kucheza mechi 16 na kufunga goli moja pekee. Balotelli analaumi mbinu za kocha wa Liverpool Brendan Rodgers ndio zimemfanya ashindwe kufanya vizuri msimu uliopita.
“Lazima
nikubali makosa yangu, mfumo uliyokuwa umechaguliwa na Rodgers
haukuendana na mimi, wakati naanza nilikosa nafasi kadhaa za wazi,
nilikuwa na nafasi chache za kufunga kwa bahati mbaya ukichanganya na
majeruhi, sikulalamika niliheshimu maamuzi ya mwalimu na nilijiheshimu
kama mchezaji professional”>>> Balotelli
“Tabia
zangu sio tu kwa sababu nimekuja Milan hata wakati nipo Liverpool mfumo
wa maisha yangu na tabia zangu zilikuwa kawaida, kwa mfano mwaka
uliopita sikuwa na tatizo lolote katika maisha yangu binafsi zaidi ya
kupiga picha nikiwa kwenye migahawa na kuweka Instagram lakini hiyo
haikuwa na maana kuwa sikuwa nikifanya mazoezi lakini
sikucheza”>>> Balotelli
“Nimeambiwa
nibadilike nifuate mfumo wa Milan nitafanya hivyo bila tatizo lolote,
nimekuwa na staili hii ya nywele kwa muda mrefu ila sitaendelea nayo
tena, matatizo yangu hayakuwa ubora wangu ila tabia nimekuwa nikiambiwa
maneno mengi sana”>>> Balotelli
Mario Balotelli amerudi AC Milan ya Italia ikiwa ni baada ya kuondoka msimu uliopita na kujiunga na Liverpool kwa ada ya uhamisho ya pound milioni 16 amerudi AC Milan akitokea Liverpool kwa mkopo wa muda mrefu.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment