HADITHI hii inaletwa kwenu kwa hisani kubwa na Mkombozi Sanitarium Clinic, Mabingwa wa tiba na magonjwa yaliyoshindikana. Mkombozi wako na mashine za kisasa za kugundua magonjwa yaliyojificha na kutoa tiba za uhakika. Mkombozi wako Chuda Tanga mkabala na kampuni ya usafirishaji abiria ya Raha Leo. simu 0654 361333
NILIJUA NIMEUA
ILIPOISHIA
Nilipomtazama vizuri
nikamgundua. Alikuwa ni Rita, dada yake marehemu mke wangu. Udugu wao ulikuwa
ni wa shangazi kwa mjomba.
Nilipooana na Halima yeye
ndiye aliyekuwa mstari wa mbele kusimamia harusi yetu.
“Oh kumbe ni wewe shemeji!”
nikamwambia na kumuuliza “Umekuja saa ngapi?”
“Nimekuja sasa hivi, nikakuta
mlango upo wazi. Naingia ndani sikuti mtu”
“Ah nilikuwa nimetoka mara
moja, nilisahau kufunga mlango”
“Huogopi waizi?”
“Nilisahau tu, si unajua
mambo ni mengi kichwani”
“Eh shauri yenu, mtakuja lia
kilio cha m’bwa!. Yuko wapi mwenzako?”
SASA ENDELEA
Nilipomtazama vizuri
nikamgundua. Alikuwa ni Rita, dada yake marehemu mke wangu. Udugu wao ulikuwa
ni wa shangazi kwa mjomba.
Nilipooana na Halima yeye
ndiye aliyekuwa mstari wa mbele kusimamia harusi yetu.
“Oh kumbe ni wewe shemeji!”
nikamwambia na kumuuliza “Umekuja saa ngapi?”
“Nimekuja sasa hivi, nikakuta
mlango upo wazi. Naingia ndani sikuti mtu”
“Ah nilikuwa nimetoka mara
moja, nilisahau kufunga mlango”
“Huogopi waizi?”
“Nilisahau tu, si unajua
mambo ni mengi kichwani”
“Eh shauri yenu, mtakuja lia
kilio cha m’bwa!. Yuko wapi mwenzako?”
Jibu nilikuwa ninalo.
“Amekwenda Pongwe” nilimjibu
haraka.
“Amekwenda saa ngapi? Si
amenipigia simu nikitoka Habours Club nije hapa”
Rita akanikwamisha.
“Amekupigia simu saa ngapi?”
“Kama
saa moja hivi. Nikamwambia nitakwenda Habours Club, jahazi wanapiga leo.
Akaniambia nikitoka huko nimfuate”
“Alikwambia anakuitia nini?”
“Sikumuuliza, nilimwambia tu
nitakuja”
“Basi aliondoka muda huo huo
kwenda Pongwe, labda alitaka akuage”
“Sasa kwanini hakuniambia kama anaondoka”
“Labda alisahau, si unamjua
mdogo wako kwa wahaka!”
“Akili gani! Wewe unajua kuwa
unasafari halafu unaniambia nije kwako? Ameniudhi kweli”
“Basi msamehe mdogo wako”
“Tena ngoja nimpigie
nimwambie nimeshakuja hapa”
“Saa hizi atakuwa amelala,
anaweza kuzima simu. Mpigie kesho”
Nilimwambia hivyo Rita kwa
sababu simu ya Halima ilikuwa pale pale kwenye kochi alipokuwa ameketi. Kama
ataipiga ingeita palepale na Rita angeniona mimi ni muongo.
Rita hata hakunisikiliza.
Alitoa simu yake kwenye mkoba akapiga na kuiweka simu sikioni.
“Kama
kazima simu nitampigia kesho” akajisemea huku akiisikiliza.
Nikawa nimemtumbulia macho
nikimuangalia.
“Inaita!” akasema.
Ghafla simu ya Halima
iliyokuwa kwenye kochi
ikaanza kuita.
Halima akageuza macho na
kuitazma
“Siumu yake si ile pale?”
Nikajifanya nashituka.
“Ah! Ameisahau…”
“Yaani amekwenda bila simu?”
“Yule msichana ana wahaka sana, ameisahau. Na mimi
ndio naiona sasa hivi”
Rita akakata simu na
kuirudisha mkobani.
“Basi naenda zangu, nipeleke”
“Sawa. Nitakupeleka”
nilimkubalia haraka ili aondoke.
Ghafla akaliona shati langu.
“Mbona shati lako lina damu
hivi?” akaniuliza kwa mshangao.
Nikagutuka na kulitazama
shati langu. Kweli lilikuwa limeingia matone makubwa ya damu ya mke wangu.
Sikuwa nimeyaona tangu mwanzo kwa sababu ya wahaka wa kuiondoa ile maiti.
Jinsi nilivyogutuka moyo
ukawa unanienda mbio.
“Hiyo damu inatoka wapi?”
Rita akaniuliza tena, sasa akiwa amekunja uso.
“Nilichinja kuku usiku huu
akanitia damu. Nilisahau kubadili shati” nikasema uongo.
“Ulimchinja wapi kuku huyo?”
“Huko uani”
“Pia nimekuta damu nyingi
huko uani, nikashangaa”
Moyo wangu ukalipuka.
“Ni damu ya kuku
niliyemchinja. Nilimchinja hapo hapo”
“Ni damu ya kuku ile? Mbona ni nyingi sana, imenishitua”
“Kuku mwenyewe alikuwa jogoo
mkubwa. Ngoja nikupeleke nije nipige deki”
Kumbe ningechelewa kidogo tu
ile maiti ingekutwa humu ndani, nikawaza huku nikielekea chumbani kubadili lile
shati.
“Sasa unaenda wapi tena?”
Rita akaniuliza.
“Nabadili hili shati mara
moja”
“Mimi nakusubiri kwenye gari”
“Sawa nisubiri”
ITAENDELEA kesho na usikose nini kitajitokeza katika mfulululizo wa hadiyhi hii hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment