Saturday, August 29, 2015

YASIKUPITE MATOKEO YA LIKU KUU ENGLAND

Nimekusogezea matokeo ya Arsenal vs Newcastle na Man City vs Watford

Ikiwa imeshinda mechi tatu mfululizo katika msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza, klabu ya Manchester City leo imeendelea kuilinda rekodi yake ya kushinda kwa 100% katika mfululizo wa mechi BPL.
 
Wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Etihad, City wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya timu iliyopanda daraja la Watford.
 
Raheem Sterling aliyenunuliwa kwa ada ya £49m kutoka Liverpool jana alifunga goli la kwanza katika msimu mpya Barclays Premier League na Fernadinho akifunga goli lingine.
Arsenal vs Newcastle  
Goli pekee lilofungwa na Alexander Chamberlain lilitosha kuipa Arsenal ushindi dhidi ya timu ngumu ya Newcastle katika mchezo uliofanyika mapema leo mchana katika uwanja wa St James Park.

No comments:

Post a Comment