Unakaribishwa kucheki na hizi barabara zenye uwezo wa kuchaji gari linalotembea…
Teknolojia imefanikiwa kuleta mambo
mapya karibu kwenye kila kitu, tumezoea kuona magari yanatumia petrol na
diesel, yakagunduliwa magari yanayotumia gesi, sasahivi yapo mpaka
yanayotumia umeme !!
Huenda kama una safari ndefu na gari
lako linatumia umeme ukapata stress nyingine, kwa mfano gari likiisha
chaji katikati ya safari inakuwaje??
Teknolojia imefika pazuri,
tunatambulishwa kwenye hizi barabara mpya, za kisasa kabisa ambazo kama
unaendesha gari inayotumia umeme basi ukipita kwenye upande huo wa
barabara gari inaendelea kuingiza chaji huku safari yako ikiendelea kwa
amani zote kabisa !!
Kwenye Jiji la Gumi, Korea Kusini
kuna mabasi ya abiria ambayo yanatumia mfumo wa umeme, wao wameweka
switch kwa ajili ya magari yanayotembea umbali wa kama Kilometa 25
wanakutana na cable za umeme kwa ajili ya kuchajia gari, hizo cable
zimepitishwa chinichini na umeme wake.
Uingereza wako kwenye mipango kuweka
hizo cable kila baada ya umbali wa kama Kilometa 32 hivi, ila mpango
mkubwa zaidi walionao ni huu wa kuanza kutumia hizo barabara ambapo
hakuna gari nyingine itaruhusiwa kupita upande huo wa barabara.
Utaalam mwingi sana uko hapo aisee,
unaambiwa gari haitasimama ili kuingiza chaji wala haitachomekwa cable
za umeme.. chaji itaendelea kujaa kwenye gari kama inavyochaji simu kwa
mfumo wa Wireless !!
Kuna sehemu tayari ndani ya Uingereza
wamekamilisha ujenzi wa barabara hizo na majaribio yatafanyika muda si
mrefu ndani ya mwaka huuhuu 2015… Unatamani hii ifike na Bongo mtu
wangu?
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment