Tuesday, August 25, 2015

MCHEZAJI WA LIGI KUU YA UINGEREZA MBARONI

Mchezaji wa Ligi Kuu Uingereza mbaroni kwa kosa hili

Asilimia kubwa ya sheria za kila nchi duniani huwa haziruhusu mtu kumtishia silaha au kumwambia maneno ambayo yatatafsirika kama kumtishia amani ya kumuua ni kosa kisheria hata kama umeongea kauli hiyo bila kumshikia silaha wala kitu chochote.
2B3A190C00000578-0-image-m-35_1439335348337
Mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal anayeichezea klabu ya West Ham United ya Uingereza Diafra Sakho anashikiliwa na polisi Uingereza baada ya kumtishia mpenzi wake kumuua. Diafra Sakho alikamatwa akiwa nyumbani kwake Hornchurch.
2B4BFC3100000578-3194410-image-a-8_1439373557624
Diafra Sakho akiwa na mpenzi wake Mya
Polisi bado hawajaweka wazi chanzo cha tatizo hilo. Sakho ambaye amejiunga na West Ham United ya Uingereza mwezi August mwaka jana akitokea katika klabu Metz ya Ufaransa na ameichezea West Ham United jumla ya mechi 26 na kufunga magoli 12.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment