Wednesday, August 26, 2015

WAANDISHI WAWILI MAREKANI WAPIGWA RISASI NA KUFA

Waandishi 2 wauawa wakiwa hewani Marekani


Waandishi wawili wa habari wamepigwa risasi katika jimbo la Marekani la Virginia wakati wakifanya mahojiano ya moja kwa moja ya runinga.
Kanda ya video inaonyesha mwandishi wa habari wa kike akimtania mgeni aliyekua akimuhoji kabla ya risasi kufyatuliwa.
Mwandishi huyo anaonekana akiruka na kamera kuanguka sakafuni huku mwanamume aliyevalia nguo nyeusi na kubeba bunduki akipita karibu.
Kituo kilichoajiri waandishi hao cha WDBJ kinasema mwandishi huyo wa habari Alison Parker na mpiga picha Adam Ward walikufa katika tukio hilo .
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment