Matusi mitandaoni Tanzania mwisho ilikua jana saa tano na dk 59 usiku ! fahamu mengine ya sheria mpya hapa
Unaambiwa mwisho wa yote ulikua jana August 31 2015 sababu leo September 1 2015 sheria hii ndio imeanza kutumika rasmi baada ya kupitishwa na Bunge mapema 2015 na kusainiwa na Rais Kikwete ikiwa ni miongoni mwa sheria zilizopitishwa na bunge kwa hati ya dharura.
Unafahamu sehemu ya makosa ambayo yanaweza kukufanya ushtakiwe?
- Kuweka mtandaoni picha za kingono za watoto
- Kuweka mtandaoni picha za ngono au za utupu
- Kuweka taarifa za uongo mtandaoni
- Kuweka taarifa za uchochezi mtandaoni
- Kutukana au kumdhalilisha mtu
- Kuweka mtandaoni tetesi zisizothibitishwa
- Kutukana au kumdhalilisha mtu kwa misingi ya udini/ukabila.
‘Sisi kama TCRA tunaweza kuitwa kama mashahidi kwenye hizo kesi, kwahiyo kuanzia August 31 2015 yale maswala ya mazoea ya NATUMA KAMA NILIVYOPOKEA au NINALETA KAMA NILIVYOIOKOTA HUKO, jihadhari sana kwa mfano yule aliyetengeneza amempelekea mtu mmoja lakini wewe umesambaza kwenye group lako la Whatsapp mko 100, utashtakiwa‘ – Innocent Mungi
No comments:
Post a Comment