Thursday, August 27, 2015

WENGER AWATULIZA MZUKA WASHABIKI WA ARSENAL

Ninayo kauli ya Arsene Wenger kuhusu suala la usajili katika klabu ya Arsenal…..

Kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger ambaye amekuwa akiwakwaza mashabiki wa klabu hiyo kwa tabia yake ya kutopenda kutoa fedha nyingi ili apate mchezaji wa kiwango cha juu, Wenger ni kocha ambaye amekuwa na misimamo ya kutopenda kununua wachezaji kwa gharama ya juu.
Arsene Wenger
Hii ni taarifa kutoka kwake kwani baada kutokubali kukiri wazi kuwa ana mpango wa kufanya usajili msimu huu, August 27 imebidi aweke wazi kama sehemu ya kuwatuliza jazba mashabiki wa timu ambao walikuwa wakiamini kuwa huenda kocha huyo hana mpango wa kusajili tena msimu huu.
“Nipo bize masaa 24 kwa siku nina team inayonizunguuka inafanya kazi usiku na mchana kutafuta ufumbuzi wa suala hili lakini bado hatuko karibu kumsajili mchezaji yoyote. Wapo maalum ambao umewalenga wanaweza kupatikana kwa sababu ya vitu fulani lakini najiamini hadi dakika ya mwisho tutakuwa tumepata ufumbuzi” >>> Wenger
Arsene Wenger
Hadi hivi sasa Arsene Wenger amefanya usajili wa golikipa Peter Cech kutokea katika klabu ya Chelsea hivyo mashabiki wa Arsenal wanamashaka kwani bado wiki moja dirisha la usajili lifungwe.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment