Saturday, August 22, 2015

SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO, AUG 22 TZ

Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha candle Education Centre Tanga, kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu. Kituo pia kinatoa kozi mbalimbali za kielimu na kiufundi ukiwemo Umeme na Computer. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746

maxresdefault
MTANZANIA
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Vijijini kwa tiketi ya CHADEMA, Patrobas Katambi amevamiwa na kundi la watu wasiofahamika, wamemnyang’anywa Fomu yake ya Ubunge na kuichana.
Kamanda wa Polisi Shinyanga, Justis Kamugisha amethibitisha tukio hilo huku akisema tukio hilo lilitokea wakati Mgombea huyo akiwa kwenye gari lake lililokuwa likiendeshwa na mdogo wake.
Vijana hao walimvamia, wakamtukana matusi na kumpora Fomu hizo pamoja na Fedha Ths, Milioni 2, Mgombea huyo hakuumizwa wala kudhurika chochote wakati wa tukio hilo.
Mgombea huyo amesema Fomu zilizochanwa zilikuwa ni kivuli (Photocopy), lakini Fomu halisi zilikuwa chini ya siti ya gari ambapo vijana hao hawakuziona.
MWANANCHI
Jeshi la Polisi Tanzania limevipiga marufuku Vikosi vya Ulinzi vya Vyama vya kisiasa kufanya kazi za ulinzi hadharani kwa madai kuwa  vinaingilia majukumu yao.
Onyo hilo limetolewa na Kamishna wa Polisi–Operesheni na Mfunzo, Paul Chagonja huku akivitaja baadhi ya Vikundi hivyo kuwa ni Green Guard (CCM), Red Brigade (CHADEMA) na Blue Guard (CUF), ambavyo hutumiwa na vyama vya siasa katika mikutano yao.
Agizo la Chagonja limekuja miezi minne baada ya agizo la Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu kupiga marufuku vikundi hivyo vya vyama vya siasa ambavyo vina muonekano na muundo wa vyombo vya usalama.
Polisi imejipanga  vizuri kuhakikisha mikutano  ya kampeni ya vyama vya siasa  inafanyika katika hali ya utulivu hadi siku ya uchaguzi,“ alisema Kamishna Chagonja.
Akizungumza hatua hiyo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alisema kuwa askari polisi hawatoshi kulinda mkutano wa watu wengi hivyo wataendelea kuwatumia kulinda wanachama wao.
Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema katika chama chao hakuna kikundi kinachoitwa Green Guard kwani hata Katiba ya chama hicho hakina watu kama hao.
Mkurugenzi wa uchaguzi wa Chama cha CUF, Shaweji Mketo alisisitiza chama chake kuendelea kuwatumia kwa sababu wapo kikatiba na katiba yao ilipitishwa na Serikali na inatambuliwa na msajili wa vyama vya siasa.
MWANANCHI
Mwanafunzi wa kidato cha pili wa Sekondari ya Nyasubi Shinyanga, Ally Jacob ameuawa baada kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni alipokuwa akijaribu kumwokoa mwanafunzi mwenzake asibakwe.
Tukio hilo lilitokea wakati mwanafunzi huyo alipokuwa akirejea nyumbani kutokea shuleni… Kamanda wa Polisi Shinyanga, Justus Kamugisha alidai kuwa mwanafunzi huyo aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya shingoni na mwenzake anayesoma Sekondari ya Kishimba.
Kamugisha alisema sababu za Jacob kuuawa ni kujaribu kumsaidia mwanafunzi mwenzake mwenye umri wa miaka 16 ambaye anasoma kidato cha pili Sekondari ya Nyasubi ili asibakwe na mtuhumiwa ambaye alitaka kufanya unyama huo kwa kushirikiana na mkazi mmoja wa Nyasubi.
Alisema watuhumiwa wote wamekamatwa na watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
NIPASHE
Wakati Mgombea Urais kupitia CCM, Dk. John Magufuli, akitarajiwa kuzindua kampeni zake kesho Dar es Salaam, mgombea kupitia Umoja wa Vyama vya UKAWA, Edward Lowassa amekwama kuzindua kampeni zake jana kama ilivyotangazwa.
Vyama vya UKAWA umeahirisha uzinduzi kutokana na kukosa mahali patakapotosha watu watakaohudhuria Uzinduzi huo.
Lowassa alitarajiwa kufungua pazia kwa kuzindua kampeni zake kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa Jijini Dar es Salaam, lakini serikali imekataza Uwanja huo kutumika kwa kampeni za vyama vya Siasa.
Kampeni zinazoanza kesho  pia zitahusisha wagombea Urais kupitia vyama vingine vya siasa vikiwamo ambavyo wagombea wake hawapewi nafasi kubwa ya kuibua ushindani kama itakavyokuwa ama kukaribia kwa CCM na UKAWA.
Alisema kuahirishwa kwa uzinduzi huo kunalenga la kutoa fursa kwa UKAWA kujiweka sawa hasa katika kupata Uwanja wenye uwezo wa kuwajumuisha watu wengi na nafasi za kuegesha magari.
Kutangazwa kwa Esther Bulaya kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo la Bunda Mjini CHADEMA kumesababisha uongozi wa jimbo wa chama hicho ‘kubomoka’ na kutangaza kumuunga mkono mgombea wa CCM, Stephen Wassira.
Mpasuko huo ulidaiwa kusababishwa na uongozi wa ngazi za juu kumpitisha Bulaya kugombea jimbo hilo wakati alishindwa kwenye kura za maoni, hivyo kufanya mwenyekiti wa wilaya, Samwel Alfred, katibu wake, Rita Itandilo na katibu mwenezi wa chama kujiuzulu nafasi zao.
Baadhi ya viongozi na wanachama wa chama hicho walisema watamuunga mkono mgombea wa CCM, Stephen Wassira kwa sababu viongozi wao wamejichanganya na kuwafanyia maamuzi yasiyo sahihi.
Hata hivyo akizungumza kwa niaba ya Katibu wa Wilaya CHADEMA, Kaunya Yohana alisema viongozi 11 waliotangaza kujiuzulu ni wazushi kwa kuwa chama kimewasimisha uongozi kwa sababu mbalimbali zikiwamo za kupandikiza mamluki, rushwa na ukiukaji wa maadili.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment