Monday, August 31, 2015

NUNDU TANGAMANO, TANGA


Tangakumekuchablog

Tanga,MGOMBEA Ubunge jimbo la Tanga mjini, Omari Nundu (CCM), amesema endapo atachaguliwa kuwa Mbunge atahakikisha kero ya upatikanaji  maji na umeme vijijini linapatiwa ufumbuzi na kudai kuwa kutokuwepo kw ahuduma hizo imekuwa chanzo cha umasikini.

Akihutubia katika ufunguzi wa kampeni kwa Wilaya ya Tanga jana, Nundu alisema maji na umeme ni kero kubwa kwa wakazi wa vijijini na hivyo kusema kuwa ndani ya Ubunge wake miaka mitano atahakikisha kero hiyo inamalizwa.

Alisema mbali ya jitihada za Serikali kupelekea umeme katika maeneo mengi ya vijijini lakini bado kuna vijiji huduma hiyo haijawafikia na kushindwa kufanya kazi za maendeleo ikiwemo ya kukoboa nafaka na kuhifadhi vyakula.

“Ndugu zangu na wanachama wenzangu wa chama cha mapinduzi nawaomba munipigie kura nyingi za ushindi ili niweze kukamilisha adhama yangu ya kupeleka umeme na maji vijijini” alisema Nundu na kuongeza

“Sote tunatambua kuwa huwezi kufikia maendeleo kama huna umeme na maji---vitu hivi ni muhimu sana kwa mustakabali wa maisha ya binadamu  kila siku hivyo nawaomba munichagua tuweze kufikia malengo yetu” alisema

Akimnadi mgombea huyo wa Ubunge, Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Henry   Shekifu aliwataka wananchi wa jimbo la Tanga kuhakikisha kura zao wanazipeleka kwa Nundu kwa madai kuwa uwezo wa kuwaletea maendeleo yuko nao.

Aliwataka  kupeleka kura zao kwa wingi  kwa mgombea wa Ubunge na Madiwani wa CCM na kusema uchaguzi huu chama hicho kinataka kuongeza idadi ya viti vya Udiwani kwa kunyakua kata ambazo zimeshikiliwa na wapinzani.

“Kura zetu zote tuzipeleke kwa mbunge na madiwani wa CCM kwani ndio chama ambacho kina sera nzuri zinazotekelezeka----mumeona mambo yaliyofanya na chama hivyo nawaomba mukipatie kura nyingi” alisema Shekifu

Aliwataka kuzitunza vitambulisho vya kupigia kura il kuweza kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Rais, Ubunge na Madiwani na kuacha kudanganywa na watu kuelekea uchaguzi na kukosa haki ya kupiga kura.

                                                   Mwisho







 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa, Henry Shekifu,akimnadi mgombea nafasi ya Ubunge jimbo la Tanga mjini , Omar Nundu, wakati wa uzinduzi wa kampeni zilizozinduliwa uwanja wa Tangamano.
 Washabiki wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) wakifurahia jambo  wakati wa uzindizi wa kampeni jimbo la Tanga za chama hicho uwanja wa Tangamano ambapo mgombea Ubunge Tanga mjini, Omar Nundu alihutubia .

No comments:

Post a Comment