Thursday, August 27, 2015

MBIO ZA UBUNGE TANGA ZAPAMBA MOTO


Tangakumekuchablog

Tanga,MGOMBEA Ubunge jimbo la Tanga mjini kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Mussa Mbarouk, amesema endapo atachaguliwa kuwa Mbunge atahakikisha shule zote inarejesha utaratibu wa uji kwa wananfunzi shuleni.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara jioni hii viwanja vya Tropicana wakati kampeni za mbio za Ubunge, Mussa alisema kuondoshwa kwa uji mashuleni imekuwa chanzo cha wanafunzi kufanya vibaya katika mitihani yao ya Taifa na mwisho wa mwaka.

Alisema utaratibu wa utoaji uji ulikuwa msaada kwa wanafunzi hata wale ambao wazazi wao wako katika mazingira magumu na hivyo kuahidi kuurejesha kwa kushirikiana na Madiwani kupitia Mabaraza ya Madiwani.

“Zamani wakati utaratibu wa uji shuleni wanafunzi walikuwa hawalalamiki njaa darasani----fahamu zao zilikuwa mzuri lakini angalia sasa  matokeo ya mitihani ya darasani na mwisho wa mwaka ni balaa” alisema Mussa na kuongeza

“Mukinichagua mimi kuwa bunge  wetu nitahakikisha shule zote za jimbo langu utaratibu wa uji mashuleni unarejeshwa----nitashirikiana na madiwani kupitia mabaraza ya halmashauri kwa pamoja kulifanikisha jambo hilo” alisema

Awali akizungumza katika mkutano huo, Diwani wa Mwanzange (CUF), Rashid Jumbe, aliwataka wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi siku ya upigaji kura na kutunza vitambulisho vyao vya kupiga kura.

Aliwataka kuvitunza  vitambulisho vyao na kuepuka kushawishiwa au kununuliwa kwani kufanya hivyo kutawakosesha haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanaowataka.

‘Ndugu zangu tunaelekea katika uchaguzi mkuu ambao mwaka huu dalili zinaonyesha tutashindwa tena kwa kishindo----vitambulisho vyenu vitunzeni katika makabati na musitembee navyo vikapotea na kukosa haki ya kupiga kura” alisema Jumbe

Aliwataka siku ya kupiga kura kuhakikisha taratibu zinafuatwa ikiwa na pamoja na mara baada ya kupiga kura kurejea katika shughuli za kujiletea maendeleo na kusbiri utangazaji wa matokeo.

                                                     Mwisho



 Mombea Ubunge jimbo la  Tanga mjini, Mussa Mbarouk, akiwahutubia wapenzi na washabiki wa chama hicho jioni hii viwanja vya Tropicana Tanga

No comments:

Post a Comment