Kwenye 255 ya leo ndani ya Show ya XXL kupitia , info ya kwanza kusikika ni la Miss universe Tz, Carolyne Bernard
kushindwa kutuwakilisha kwenye mashindano hayo Kidunia kutokana na
matatizo ya kiafya, na badala yake inabini mshindi wa pili Nale Boniface
kutuwakilisha, leo muandaaji wa mashindano hayo Maria Sarungi amesema, walimpeleka katika Hospitali ya MOI na kupatiwa matibabu, Kutokana na hali hiyo, Nale Boniface
ambaye alishika nafasi ya pili na kuiwakilisha Tanzania katika
mashindano ya Miss Earth ndiye atakayekwenda kuiwakilisha nchi badala
yake kama mkataba unavyoainisha na hivyo atakuwa Miss Universe Tanzania
2014, Mashindano ya Miss Universe Tanzania mwaka huu yalifanyika tarehe
31 mwezi wa kumi.Studio ya DM record Arusha imehamishia makazi yake Dar ambapo Producer wa studio hiyo Regi amesema lengo la kuhamisha ni kufikia malengo yao waliyojiwekea wakati wanaanzisha ikiwemo kufikia watu wengi, wameshafanya kazi Arusha wamejulikana wakaamua kupanua wigo wa kusikika zaidi kwa kuja Dar.
Diamond jana amepost picha akiwa Ikulu Dar akiwa na Rais Jakaya Kikwete, mezani kukiwa na tuzo tatu za Channel 0, 255 jana ilitoa Info juu ya mwakilishi wa TZ na mshindi wa BBA 2014, Idris ambae alitarajiwa kuwa Ikulu kwa mwaliko maalum wa Rais, lakini kutokana na sababu zisizozuilika ikabidi safari hiyo iyairishwe, Idris alikuwa ameandika ujumbe katika mtandao wake wa twitter akiwaambia mafans wake waandike ujumbe wowote wanaotaka ufike kwa Rais, amesema watu waliandika vitu vingi, ikiwemo watu wengi kuzungumzia swala la Escrow jambo ambalo linaonekana kuwakera watu wengi, ratiba itakapopangwa tena Idris ataenda Ikulu akiwa na ujumbe wa kuwainua Vijana
No comments:
Post a Comment