Hekaheka ya leo December 24 iko hapa, ni muendelezo wa ile ya msichana aliyemtupa mtoto chooni.
Hekaheka
ya leo December 24, ni muendelezo wa ile ya Desembar 16, iliyokuwa
inatoka Dar es Salaam ambapo msichana mmoja alijifungua mtoto chumbani
kwake ndani ya nyumba aliyopanga na kwenda kumtupa mtoto ndani ya shimo
la choo huku akieleza kuwa sababu iliyomfanya aamue kufanya hivyo ni
kitendo cha mwanaume aliyempa ujauzito huo kumtelekeza.Baada ya majirani kufanikiwa kumtoa mtoto huyo akiwa mzima na kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala, kwenye mwendelezo wa Hekaheka ya leo Taarifa zinasema kuwa kwa sasa mtoto huyo amehamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi, Mjumbe wa eneo analokaa binti huyo, ambae amekuwa akimsaidia binti huyo amesema hali ya Mama na Mtoto wanaendelea vizuri ingawa mtoto bado hajaongezeka uzito, na kuelezea masikitiko yake kuhusu mama wa mtoto kukataa kuwa wazi kuhusu ndugu zake walipo kitendo ambacho kinawafanya washindwe kumsaidia na walipomtaka kumrudisha kwao Tanga Makorora binti huyo aliktaa.
No comments:
Post a Comment