Alikataliwa kumuoa binti ambaye ni binamu yake, kilichotokea ni hiki kilichofikia mpaka headlines za dunia.

Basi hii imetokea Pakistani ambako Gul
Ahmed Said amemuua Baba Mkwe mtarajiwa pamoja na watu wengine tisa wa
familia yake baada ya kukataliwa kumuoa Binti wa Mzee huyo huko
Charsadda.
Binti aliekua anataka kumuoa ni binamu yake
ambapo Polisi wa Pakistani wamesema ugomvi ulianzia kwenye mabishano ya
idadi ya dhahabu kwenye harusi.
Waliouwawa kwa risasi ni Watoto nane wa
mzee huyo, mzee mwenyewe pamoja na mke wake ambapo Polisi bado
wanaendelea kumtafuta Said ambaye amekua akitafutwa kutokana na mauaji
mengine aliyoyafanya November 2014 kwa kuwaua Wazazi wake, kaka yake
pamoja na shemeji yake.
No comments:
Post a Comment