Tuesday, April 7, 2015

TEKNOLOJIA YA CHAJI YA SIMU

Sasa hivi teknolojia inatuletea hii.. simu yako itajaa chaji kwa dakika moja tu !

summer-camper-low-battery
Kwa sababu unahitaji mawasiliano lazima uwe na simu.. Kwa kuwa unahitaji mawasiliano bora na ya kisasa labda ukajikuta unalazimika kuwa na smartphone.. Watu wengi wanapenda kutumia smartphone kwa kuwa inarahisisha vingi.. Facebook, Twitter, Whatsapp unatumia kiurahisi kabisa.
Baada ya hapo ikaja teknolojia ya kifaa cha kutunzia umeme ili kama mtu ukiishiwa chaji kwenye simu yako na uko mbali basi Power bank inasaidia simu yako kuendelea kuwa hewani kwa muda mrefu zaidi.
GOOD NEWS kwako, huenda muda mfupi ujao usihitaji sana kutembea na Power bank yako.
Utafiti umefanyika  Stanford University California ambapo wamebuni betri aina nyingine ambayo hii unaambiwa inajaa chaji kwa dakika moja tu.. ni rahisi zaidi na salama kuitumia hii.
Wanasayansi wanasema hii betri itakuwa salama zaidi kwa kuwa hailipuki kama ambavyo ziko betri nyingi zinazotumiwa sasa hivi ambazo zimetengezwa kwa lithium.
Utaenjoy sana hii kwa sababu inajaa chaji kwa haraka zaidi, japo betri hii inaisha kwa haraka ukilinganisha na betri hizi za kawaida.. ila kama ukipata betri hii hautohitaji kukaa muda mrefu kusubiri simu yako ijae chaji kwenye umeme.

Kaa karibu na www.tangakumekucha.blogspot.com nitakachokipata nitakusogezea hapa muda wowote kuanzia sasa, usikae mbali.

No comments:

Post a Comment