Thursday, April 9, 2015

APRIL 09 NI VILIO KILA KONA

Baada ya ajali ya Tanga, hii nyingine ni MOROGORO leoleo… Watu wengine wamefariki na kujeruhiwa.

IMG-20150409-WA0015Mara nyingi stori za aina hii huanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, baadae unaona RADIO na TV nazo zinaanza kuripoti.. Siku ya leo APRIL 9 watu walianza kusambaziana picha za ajali iliyotokea Tanga, mabasi mawili ya abiria na gari dogo yamegongana, watu 10 wamefariki na wengine kujeruhiwa.. kabla siku haijaisha naipokea hii nyingine kutoka Morogoro.
Basi la Kampuni ya Happy Nation lenye namba T 618 BDN lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Mbeya katika eneo la Mikumi, Morogoro.. taarifa za awali zinasema watu wawili wamefariki na wengine kujeruhiwa.
IMG-20150409-WA0013

Chanzo cha ajali hakijafahamika, naifuatilia hii kwa ukaribu.. kitakachonifikia nitakusogezea hapa muda wowote mtu wangu.
IMG-20150409-WA0014
IMG-20150409-WA0015
Tangakumekucha inafuatilia kwa karibu matukio ya Tanga na Morogoro hivyo kuwa karibu nami nitakusogezea kila kinachonifia ni hapa hapa

No comments:

Post a Comment