Kumbe Charles Hillary kaondoka BBC na kuamua kurudi nyumbani?
Miongoni mwa watu ambao sauti zao zimesikika sana kupitia BBC London, ni Mtangazaji Mtanzania Charles Hillary aliyewahi kusikika sana hata kupitia Radio One pia.
Charles Hillary sasa anarudi nyumbani 
Tanzania na kujiunga na kituo cha Televisheni cha Azam ambapo mhariri wa
 BBC Afrika Dar es salaam Solomon Mugera aliwaambia wafanyakazi wake kuhusu kuondoka kwa Hillary.
Naibu Mtendaji mkuu wa Azam Tido Mhando
 alithibitisha Hillary kutarajiwa kujiunga na Azam Media akiwa na 
historia nzuri kwenye vyombo vya habari kuanzia alipoanza mwaka 1994 
Radio one na kabla ya hapo alitokea radio Deutsch Welle na mwaka 2006 alijiunga na BBC.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:
Post a Comment