Wazazi waliingilia ndoa ya mtoto wao, mkwe akaona alipize kisasi kwenye chai
Migogoro
 kwenye ndoa wengine wanaona ni kawaida, wengine huwa inawachosha.. Ziko
 story utasikia wanandoa wamepigana, wengine wanaachana.
Nimeipata hii stori toka India, Rekha Nagvanshi ni mwanamke ambaye ameonekana kuchoshwa na manyanyaso ya mume wake, kuna wakati waliachana.. baadae wakarudiana.
Baada ya kurudiana makubaliano ilikuwa 
hivi, mume awe anahusika na majukumu yote ya nyumbani yani kuanzia kufua
 nguo, kuosha vyombo.. kupika.
Wazazi waliingilia kati na kufanya makubaliano hayo yakavunjika, Rekha hakuridhika wazazi kuingilia kati masuala yao ya ndoa.
Rekha alikutwa na mama mkwe wake 
akikojolea kwenye birika la chai jikoni, rafiki yake anasema labda kwa 
vile alikasirishwa na wazazi hao ndio maana akaamua alipize kisasi kwa 
kufanya hivyo.
Wazazi hao wamesema walikuwa wanajua 
mkwe wao hawapendi lakini hawakufikiria kama angeweza kuwafanyia kitendo
 hicho, walienda kutoa taarifa Polisi lakini majibu ya Polisi 
waliwaambia hawashughulikii kesi za namna hiyo.
Mume wa mwanamke huyo ambaye anaitwa Deepak amesema yeye aliridhika na masharti ya mke wake waliporudiana lakini wazazi wake hawakupenda kuona anafanywa kama mtumwa.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:
Post a Comment