Mauaji ya mtu mwingine mweusi Marekani

Leo hii ni story ya Afisa mwingine wa
Polisi wa jimbo la CarolinaKusini kushtakiwa kwa mauaji, ushahidi wa
video unaonesha Askari huyo alimpiga risasi nane mgongoni mtu ambae ni
Mmarekani mweusi.
Tukio hilo limetokea Jumamosi April 4 2015 ambapo shahidi mmoja alirekodi tukio hilo kwa video inayomuonesha Marehemu Walter Scott ambaye umri wake ni miaka 5o akikimbizwa na Afisa wa Polisi mzungu aliyekuwa na bunduki, akampiga risasi nane mgongoni, Walter alipoanguka alimfunga pingu.
Afisa huyo Thomas Slager
amejitetea kuwa Mmarekani huyo mweusi alikuwa akiendesha gari,
alipomsimamisha kwa ajili ya kukaguliwa, alionekana kupingana na amri ya
Polisi, akamuibia Polisi kifaa chake ambacho huwa Askari wanakitumia
kuwapiga shoti ya umeme wahalifu, Askari huyo akaamua kumpiga risasi.
Hata hivyo Thomas Slager ameshtakiwa kwa mauaji na anakabiliwa na adhabu ya kifo au kifungo cha miaka 30 jela.
No comments:
Post a Comment