Bondia wa mwisho kumpiga Floyd Mayweather eti hana hata TV?
Floyd Mayweather anazungumziwa sana.. Bondia mkali.. ana mbwembwe zake nyingi tu kila siku, labda unajua kwamba Mayweather hajawahi kupoteza pambano hata moja tangu mwaka 1996 kwenye michezo ya Olimpiki, lakini unamjua bondia aliyempiga Mayweather yuko kwenye hali gani sasa hivi.
Usishtuke kuambiwa jamaa ni maskini na anaishi kwenye mazingira magumu sana tofauti na mnyonge wake wa zamani, Mayweather!!
Historia inamkumbuka Serafim Todorov, raia wa Bulgaria.. bondia wa mwisho kumshinda Mayweather,
wenye hizi taarifa toka nyumbani kwake kabisa wanasema jamaa hana hata
flat screen.. hiyo sio tatizo.. unaambiwa kwa sasa anaishi kwa kupokea
pensheni ambayo ni kama dola 435 kwa mwezi, sawa na 810,000/= kama
ingekuwa BONGO.
Leo hii dunia inasubiri May 2 2015 kumuona Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wakiwa ulingoni, pambano ambalo limeingia kwenye record kuwa pambano la hela nyingi zaidi kutokea duniani.. Kama ikitokea Mayweather akapigwa kuna macho ambacho yatarudisha kumbukumbu nyuma na kumcheki mbabe wa mwisho kumpiga Mayweather nae akakaa kwenye headlines kubwa kwa mara nyingine.

Ni kawaida kumuona Floyd Mayweather akiringisha pesa zake.
No comments:
Post a Comment