MTANZANIA
Wazazi wa Mtanzania Rashid Charles Mberesero (21), anayetuhumiwa kuwa mmoja wa wanamgambo wa Al-Shabaab ambao walifanya mauaji katika Chuo Kikuu cha Garissa nchini Kenya na kuua wanafunzi 148, wamefunguka na kueleza siri ya mtoto wao huyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana,
walisema wakati kijana huyo akihusishwa na tukio hilo lililotokea
Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo, walikuwa wakijua mtoto wao yupo
shuleni mkoani Dodoma.
Baba mzazi wa mtoto huyo, Charles Mberesero, alisema mwanawe huyo ni mwanafunzi wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Bihawana iliyopo mjini Dodoma.
Alisema kwa muda mrefu mtoto wake
alikuwa akilelewa na mama yake mzazi huko Gonja, Same mkoani
Kilimanjaro, lakini kwa muda mfupi alioishi naye hakuwahi kufikiri
kwamba angeweza kujihusisha na tukio kama hilo.
“Rashid
alizaliwa mwaka 1994 huko Gonja Same, shule ya msingi aliyosoma
siikumbuki, lakini sekondari najua kidato cha kwanza hadi cha nne
alisoma katika Shule ya Gonja,”Mberesero.
Akimwelezea tabia yake, alisema Rashid ni kijana mtaratibu na mvumilivu sana.
“Alipokuwa
akisoma O’ level nilikuwa nawasiliana naye sana, lakini kama mwaka
mmoja na nusu uliopita tulikuwa hatuna mawasiliano ya karibu.
“Sasa
hivi alikuwa anasoma PCB kwenye Sekondari ya Bihawana Dodoma. Kwenye
matokeo ya kidato cha nne alipata daraja la pili na michepuo yote ya
masomo ya Sayansi ilikubali, lakini akaamua kusoma PCB,”.
“Juzi
baada ya kutokea hayo yaliyotokea huko Kenya niliongea na mama yake,
akaniambia mtoto alikuwa likizo ya kama wiki mbili na Machi 21, mwaka
huu aliaga nyumbani kwamba anarudi shuleni Dodoma.
“Na
unajua mambo ya huko kijijini baada ya mtoto kusema anasafiri kwenda
Dodoma shuleni hakuna mtu aliyefuatilia hadi baadaye tulipokuja kusikia
hayo ya Kenya.”
Alisema kutokana na alivyoshtushwa na
tukio hilo, tangu alivyopata taarifa zake siku ya Jumapili, alipata
presha na jana ndipo aliweza kupata ahuweni na kutoka nyumbani.
Baba huyo alisema uhusiano wake na mtoto wake haukuwa mzuri sana kwa sababu alimtaka abadilishe dini yake akakataa.
“Nilikuwa
namshawishi afuate dini yangu, mimi ni Mkatoliki kwa hiyo kuna wakati
alikuja kwangu akakaa kama mwezi mmoja nikawa naenda naye kanisani,
nikawa namshawishi abatizwe.
“Alikataa
akasema anafuata dini ya mama yake… baada ya kuzaliwa sikumfuatilia
sana kwa sababu mama yake aliolewa na mtu mwingine, sasa pale mimi
kuzungumza naye kila saa isingewezekana,” .
Mberesero alisema kwa muda aliomjua
mtoto wake huyo, anafahamu kwamba si mtu wa kutoka sana nyumbani kwa
hiyo anashindwa kujua ni wapi alipojifunzia mambo ya kigaidi.
Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti
hili, mama mzazi wa Rashid, Fatma Ally, alisema mwaka jana mtoto wake
huyo alifaulu mtihani wa kidato cha nne na kupangiwa kujiunga na kidato
cha tano katika Shule ya Sekondari Kingwe iliyopo mkoani Dodoma.
Alisema alivyofika kwenye shule hiyo
alibaini haikuwa na mchepuo wa Sayansi aliokuwa akisoma, hivyo akaomba
kuhama na ndipo alipopata nafasi Shule ya Sekondari Bihawana.
“Hakusubiri likizo iishe, akasema kwa sababu sisi ni Waislamu haisubiri
Pasaka, nikamwandalia vitu vyake akasema anaenda shuleni,” alisema.
“Hata akiwa nyumbani akitoka sana anaenda msikitini, sijui huo ushawishi kaupata msikitini ama huko shuleni,” alisema
Alisema siku mwanaye huyo anaenda shule, alimpa Sh 90,000 kwa ajili ya nauli na matumizi mengine.
Alisema siku mwanaye huyo anaenda shule, alimpa Sh 90,000 kwa ajili ya nauli na matumizi mengine.
“Hata akiwa shuleni akiniambia ana shida
huwa namtumia fedha yoyote niliyonayo, naweza kumtumia Sh 5,000, 10,000
ama 20,000,” alisema.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Bihawana,
Mbilinyi Joseph, alithibitisha kwamba Rashid Charles Mberesero ni
mwanafunzi wa shule hiyo na tangu mwanafunzi huyo alipoondoka wakati wa
likizo Novemba 25, mwaka jana hadi sasa hajarejea shuleni.
MTANZANIA
Serikali imewasimamisha kazi vigogo watatu wa Mamlaka ya Ustawishaji Bonde la Mto Rufiji (Rubada) kwa muda usiofahamika.
Vigogo hao wamesimamishwa kazi baada ya kutuhumiwa kwa ubadhilifu wa zaidi ya Sh bilioni 2.3.
Vigogo hao wamesimamishwa kazi baada ya kutuhumiwa kwa ubadhilifu wa zaidi ya Sh bilioni 2.3.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, aliwataja vigogo hao ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Aloyce Masanja,
Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Tabu Ndatulu
na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala,Filozi Mayayi alisema ubadhilifu huo
umebainika baada ya tume iliyoundwa na wizara kwa kushirikiana na Hazina
kufanya uchunguzi wa kina.
Wasira alisema viongozi hao wamekuwa
wakijihusisha na masuala mbalimbali ya kiuongozi, jambo ambalo kamwe
Serikali haiwezi kulivumilia.
Alisema amechukua uamuzi huo wa kinidhamu kwa kutumia mamlaka yake ya waziri mwenye dhamana.
Wasira alisema makosa mengine ya kijinai ameiachia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi.
Wasira alisema makosa mengine ya kijinai ameiachia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi.
Alisema vigogo hao walikuwa wakiwatoza fedha watu ambao walikuwa wanataka kuwekeza kwenye kilimo.
“Kibaya,
hawa viongozi walikuwa wakiwatapeli wawekezaji kwenye sekta ya kilimo
kwa kuwatoza fedha bila kuwaonyesha maeneo ya kulima jambo ambalo
lilizua malalamiko makubwa,”Wasira.
Alisema zaidi ya Sh bilioni 2.7
zilipokewa na maofisa hao kutoka kwa wawekezaji, lakini fedha
zilizoonekana kwenye akaunti ni Sh milioni 714.6 wakati Sh bilioni 2.3
hazijulikani zilipo.
Wasira alisema tayari ameiandikia Bodi
ya Wakurugenzi ya Rubada ianzishe mchakato wa kujaza nafasi hizo haraka
iwezekanavyo ili kazi ziweze kuendelea kama kawaida.
“Maofisa
hawa wakuu walikuwa wakijilipa masurufu na baadhi ya fedha
zimegundulika kuwekwa kwenye akaunti zao binafsi badala ya ile ya
Rubada.
“Fedha
za wafanyakazi zaidi ya Sh milioni 58 walizokuwa wakikatwa kwa ajili ya
kupelekwa katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ziliishia
mifukoni mwao, taratibu za utoaji tenda zilikiukwa, wamefanya
watakavyo,” Wasira.
Alisema mfumo mzima wa utendaji wa
mamlaka hiyo ulikuwa dhaifu na hakukuwapo na mgawanyo wa kazi, huku
maofisa hao wakiidhinisha malipo na kutembea na fedha mifukoni.
Wasira alisema kazi hiyo ilipaswa kufanywa na mhasibu kama utaratibu wa Serikali unavyotaka.
Rais huyo wa awamu ya tatu aliyasema
hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati wa mahojiano aliyoyafanya na
vyombo vya habari kwenye Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), baada ya kutoa mhadhara kwa wanafunzi wa chuo hicho.
Mkapa alitoa mhadhara kuhusiana na tathmini ya kiuchumi kuelekea vita ya tatu ya dunia.
Mkapa alisema kwa hali ilivyo sasa ni
sababu za kiuchumi ndizo zinazoleta vita, kutokana na uongozi mbaya,
njaa na kiu ya baadhi ya nchi kutaka maliasili za mataifa mengine.
“Hatutarajii
kuwa na vita kama ile ya pili ya dunia, kwa sababu Dunia sasa inamiliki
silaha kali kama za nyuklia, zinazoweza kuangamiza maisha kwa wingi, na
ndiyo maana unaona mazungumzo kupunguza silaha za nyuklia kama yale ya
Iran,” .
Alisema ili kuzuia vita kutokea ndani ya
nchi, ama kati ya nchi mbili, ukanda, bara na hata dunia, kuna umuhimu
wa serikali zilizoko madarakani na hasa barani Afrika kuwekeza kwenye
uongozi bora na kuwashirikisha wananchi katika maamuzi ya kidemokrasia,
yanayohusu maisha na rasilimali za nchi zao.
“Ni
vizuri kuwa na sera zinazojenga, zisizogawa wananchi katika misingi ya
udini na ukabila, kuhakikisha mikataba inayoingiwa juu ya rasilimali za
nchi inawanufaisha wananchi na si wageni peke yao, na kama kuna
unahitaji wa kuirekebisha, ni bora hilo likafanyika,” .
Alisema mikataba kama ule wa EPA, si ya
kuiruhusu kwani mwisho wa siku itaua juhudi za nchi maskini kuendelea,
kwa sababu zinalenga kuifanya Afrika kuwa soko la bidhaa za Ulaya.
“Mazungumzo
juu ya EPA kwa nchi nyingi zilizo kwenye eneo la Sahara ni kama
yamemalizika, kinachosubiriwa sana sana na kuridhiwa na mabunge, lakini
mkataba huu kimsingi haufai kwa nchi zetu za Afrika,” alitahadharisha Mkapa.
Mkapa alisema: “Iwapo
EPA itaridhiwa na mataifa yetu, itakuwa ni chanzo cha kudhoofisha
kilimo chetu, viwanda vyetu, malighafi hazitasindikwa na maduka yetu
yatajaa bidhaa za Ulaya na mwisho wa siku ajira itakosekana.”
Akizungumzia suala la muundo wa sasa wa UNSC, Mkapa alisema: “Kuna umuhimu wa kuifumua taasisi hiyo kwa sababu dunia sasa imebadilika, tofauti na ilivyokuwa wakati inaundwa,”.
Alisema tasisi hiyo inastahili
kufumuliwa na kuundwa upya kwa sababu hivi sasa kuna mataifa ambayo
yameendelea sana kiuchumi na kiuwezo katika dhana za kivita na hivyo
kustahili kuwamo ndani yake.
Alisema mataifa hayo yanastahili kuwamo
ndani ya taasisi hiyo kwa sababu ya ushawishi na nafasi yaliyonayo sasa,
inayoyafanya yawe na mchango kwenye maamuzi ya taasisi hiyo.
NIPASHE
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa,
amezipa angalizo nchi za Kiafrika kukuza uongozi bora na kuachana na
mikataba mibovu isiyojali ustawi wa wananchi kwa kuwa inaweza kuzipeleka
katika vita.
Miongoni mwa mikataba ambayo amesema
kuwa ni mibovu na isiyofaa, hivyo iepukwe ni wa Kiuchumi baina ya
Mataifa ya Afrika, Caribbean na Pacific (EPA), ili kuepusha vita, ambayo
kwa sasa itakuwa ni ya kiuchumi.
Aidha, ametaka Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa (UNSC) lifumuliwe ili kuongeza nchi nyingine ambazo
zinastahili kuingia kwa sasa.
Rais huyo wa awamu ya tatu aliyasema
hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati wa mahojiano aliyoyafanya na
vyombo vya habari kwenye Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), baada ya kutoa
mhadhara kwa wanafunzi wa chuo hicho.
Mkapa alitoa mhadhara kuhusiana na tathmini ya kiuchumi kuelekea vita ya tatu ya dunia.
Mkapa alisema kwa hali ilivyo sasa ni
sababu za kiuchumi ndizo zinazoleta vita, kutokana na uongozi mbaya,
njaa na kiu ya baadhi ya nchi kutaka maliasili za mataifa mengine.
“Hatutarajii kuwa na vita kama ile ya
pili ya dunia, kwa sababu Dunia sasa inamiliki silaha kali kama za
nyuklia, zinazoweza kuangamiza maisha kwa wingi, na ndiyo maana unaona
mazungumzo kupunguza silaha za nyuklia kama yale ya Iran,” alisema.
Alisema ili kuzuia vita kutokea ndani ya
nchi, ama kati ya nchi mbili, ukanda, bara na hata dunia, kuna umuhimu
wa serikali zilizoko madarakani na hasa barani Afrika kuwekeza kwenye
uongozi bora na kuwashirikisha wananchi katika maamuzi ya kidemokrasia,
yanayohusu maisha na rasilimali za nchi zao.
“Ni vizuri kuwa na sera zinazojenga,
zisizogawa wananchi katika misingi ya udini na ukabila, kuhakikisha
mikataba inayoingiwa juu ya rasilimali za nchi inawanufaisha wananchi na
si wageni peke yao, na kama kuna unahitaji wa kuirekebisha, ni bora
hilo likafanyika,” alisema.
Alisema mikataba kama ule wa EPA, si ya
kuiruhusu kwani mwisho wa siku itaua juhudi za nchi maskini kuendelea,
kwa sababu zinalenga kuifanya Afrika kuwa soko la bidhaa za Ulaya.
“Mazungumzo juu ya EPA kwa nchi nyingi
zilizo kwenye eneo la Sahara ni kama yamemalizika, kinachosubiriwa sana
sana na kuridhiwa na mabunge, lakini mkataba huu kimsingi haufai kwa
nchi zetu za Afrika,” alitahadharisha Mkapa.
Mkapa alisema: “Iwapo EPA itaridhiwa na
mataifa yetu, itakuwa ni chanzo cha kudhoofisha kilimo chetu, viwanda
vyetu, malighafi hazitasindikwa na maduka yetu yatajaa bidhaa za Ulaya
na mwisho wa siku ajira itakosekana.”
Akizungumzia suala la muundo wa sasa wa
UNSC, Mkapa alisema: “Kuna umuhimu wa kuifumua taasisi hiyo kwa sababu
dunia sasa imebadilika, tofauti na ilivyokuwa wakati inaundwa,” alisema.
Alisema tasisi hiyo inastahili
kufumuliwa na kuundwa upya kwa sababu hivi sasa kuna mataifa ambayo
yameendelea sana kiuchumi na kiuwezo katika dhana za kivita na hivyo
kustahili kuwamo ndani yake.
Alisema mataifa hayo yanastahili kuwamo
ndani ya taasisi hiyo kwa sababu ya ushawishi na nafasi yaliyonayo sasa,
inayoyafanya yawe na mchango kwenye maamuzi ya taasisi hiyo.
NIPASHE
Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima,
anatarajiwa kuhojiwa leo na Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam
katika Kituo cha Polisi cha Kati huku wasaidizi wake wakisema afya
imeimarika na yupo tayari kwa mahojiano hayo.
Mwanasheria wa Askofu Gwajima, Paul Mallya, alisema jana kuwa mteja wake afya yake imeimarika na yupo tayari kwa mahojiano ya mwisho leo.
“Mteja
wangu anaeandelea vizuri, kesho (leo) saa mbili asubuhi atahojiwa kama
maelekezo ya mwisho ya Jeshi la Polisi yalivyomtaka aende kuhojiwa,” Mallya.
Hata hivyo, Mallya alisema hafahamu kuwa
Askofu Gwajima ataongozana na msafara wa watu wangapi huku akisistiza
kuwa anachofahamu ni kuwa mteja wake atafika kituo cha polisi cha kati
kwa ajili ya mahojiano.
Naye mmoja wa wasaidizi wa karibu wa
Askofu ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alilieleza jana kuwa
afya ya kiongozi huyo wa kiroho imeimarika na atakwenda katika
mahojiano kama ilivyopangwa, lakini alisema hafahamu ni msafara wa watu
wangapi utakaomsikdikiza.
Jitihada za kumtafuta kupitia simu yake
ya mkononi Kamanda wa Polisi wa kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman
Kova, kuzungumzia jinsi polisi walivyojipanga kiulinzi endapo Askofu
Gwajima atakwenda kituoni hapo na msafara wa waamini wake, simu yake
haikupokelewa.
Aprili 2, mwaka huu Jeshi la Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilishindwa kumhoji Askofu Gwajima
kutokana na kutoridhika na mwenendo wa afya yake, hali iliyomlazimu
kuagizwa kurudi tena leo kwa ajili ya mahojiano hayo.
Wakili Mallya, alisema Askofu Gwajima
atakwenda Polisi tena kuhojiwa kutokana na mtu aliyetambulika kwa jina
la Abubakar Yusufu, mkazi wa Kiluvya, wilaya ya Kisarawe, mkoa wa Pwani,
kufungua kesi ya jinai polisi akilalamika kukwazwa na lugha
iliyotumiwa na askofu huyo dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo
Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Alisema Yusufu alifungua mashtaka hayo
kutokana na picha ya video aliyoiona kwenye mitandao ya kijamii
inayomuonyesha Askofu Gwajima akitumia lugha ya matusi kumkashifu Askofu
Pengo ambayo kisheria ni kosa.
Machi 26, mwaka huu, Jeshi la Polisi
Kanda hiyo lilimwamuru Askofu Gwajima kujisalimilisha polisi kwa tuhuma
za kumkashifu Kardinali Pengo.
Machi 27, Askofu Gwajima alijisalimisha
kituo hicho, lakini wakati akihojiwa alizimia akiwa chumba cha mahojiano
kisha kukimbizwa katika Hospitali ya TMJ kwa matibabu.
Jumanne ya wiki iliyopita aliondolewa
TMJ na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Oyesterbay na kuachiwa bila
masharti, lakini alielekezwa kuripoti Alhamisi iliyopitwa katika Kituo
cha Polisi Kati.
NIPASHE
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Wilaya ya Morogoro, kimetangaza kufanya maandamano makubwa kwenda kwa
uongozi wa Manispaa ya Morogoro, kushinikiza kutekelezwa kauli ya
Mbunge wa Jimbo la Morogoro, Abdulaziz Abood (CCM) ya
kutaka kutolewa taarifa ya matumizi ya Sh. milioni 720 za mradi mkubwa
wa ujenzi wa stendi ya mabasi yaendayo mikoani eneo la Msamvu.
Pamoja na fedha hizo, pia Chadema
inataka maelezo mengine kutoka kwa Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Morogoro akiwamo Meya na Mkurugenzi kuhusu fedha za miradi ya ujenzi
wa soko kuu la Morogoro .
Hatua ya Chadema kuamua kufanya
maandamano hayo imekuja siku chache baada ya Abood kufanya ziara ya
kukagua mradi huo na kunyimwa taarifa za matumizi ya fedha ungozi wa
manispaa, hivyo kulazimika kuahirisha ziara hiyo, huku akitoa siku 14
taarifa hiyo itolewe vinginevyo suala hilo atalifikisha kwa Rais Jakaya
Kikwete.
Hata hivyo, uongozi wa Manispaa ya
Morogoro kupitia Meya wake, Amir Nondo ukizungumzia suala hilo kwa
waandishi wa habari, ulieleza kuwa ujenzi wa mradi unafanywa kwa ubia na
Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF) ambao ndiyo wanawajibika
na fedha hizo Sh. milioni 720 walizitoa kwa ajili ya fidia ya kumlipa
mtu aliyekuwa ndani ya eneo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari
mkoani hapa jana, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Morogoro, alisema
wanakusudia kufanya maandamano hayo Aprili 14 mwaka huu kwenda ofisi
hiyo ya mkurugenzi wa manispaa na meya kutaka matumizi ya fedha za mradi
huo wa stendi yawekwe wazi.
Alisema katika mradi huo wa ujenzi wa
stendi ya kisasa kuna harufu ya ufisadi unaofanywa na baadhi ya viongozi
wa manispaa ndiyo maana wanakataa kutoa taarifa zake kwa mbunge.
“Yule
ni mbunge anapaswa kujua maendeleo ya ujenzi sasa tunashangaa kwanini
wanamnyima taarifa za mradi ambao ni sehemu ya fedha za serikali, kama
hakuna ufisadi wanaficha nini?. Sasa sisi tutafanya mandamano ya
kumuunga mkono Abood ili wananchi wapewe taarifa za mradi huo na
maendeleo yake,” .
Mwenyekiti wa Chadema alilitaadhalisha
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro kuwa lisithubutu kuyazuia maandamano
hayo ya amani, kwani hawatakubali kuzuiliwa kwa kuwa hizo ni fedha za
wananchi ambao wengi wao wanashindwa kupata huduma nyingine kama za afya
kutokana na mradi huo.
Mradi wa stendi ya kisasa ya mabasi yaendayo mikoani ya Msamvu unatalajiwa kutumia Sh. bilioni 10 katika awamu ya kwanza.
MWANANCHI
Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe
amesema zaidi ya wabunge 50 wa vyama mbalimbali vya siasa nchini
watajiunga na chama hicho kipya na kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu
wa Oktoba mwaka huu.
Zitto ambaye alijivua ubunge wa Kigoma
Kaskazini baada ya kufukuzwa uanachama wa Chadema, amebainisha kuwa
wabunge hao, wakiwamo wa CCM na Chadema, ni miongoni mwa watu
wanaokichangia fedha chama hicho kilichopata usajili wa kudumu Mei,
mwaka jana na kuzinduliwa mwezi uliopita.
Pia, amewatangazia vita wabunge wa
majimbo manane ya Mkoa wa Kigoma, akijigamba kuwa ili waweze kuibuka na
ushindi katika uchaguzi huo ni lazima wakubali kujiunga na ACT kwa kuwa
chama hicho kimejipanga kuyabeba majimbo yote.
Akizungumza na waandishi wa Mwananchi
katika ofisi za gazeti hili, Dar es Salaam jana, Zitto alisema ACT ni
chama kilichojipanga na ndiyo maana haikuwa ajabu katika mkutano wake
mkuu wa hivi karibuni kuhudhuriwa na wanachama zaidi ya 400 na kufanya
uzinduzi wa aina yake, huku akisisitiza kuwa chama hicho kinaungwa mkono
na watu wengi.
“Tuna
wagombea ubunge wengi wakiwamo wabunge wa sasa ambao katika Uchaguzi
Mkuu Oktoba hawatagombea kupitia vyama vyao vya sasa. Wapo ambao
hawatakwenda hata katika kura za maoni za vyama vyao na wameshafanya
uamuzi,” Zitto
Huku akizungumza kwa kujiamini, Zitto
alisema wabunge hao ndiyo sababu ya chama hicho kuwa na uwezo wa
kujiendesha na kufafanua kuwa ACT kinawakaribisha wabunge na makada wote
kutoka vyama vya Chadema na CCM.
“Wale
ambao wanabanwa CCM na kukosa uhuru wa kuhoji jambo lolote hiki (ACT)
ndicho chama chao. Wale ambao wanaamini kuwa aina za siasa tulizotaka
kuzifanya ndani ya Chadema tukashindwa kuzifanya na wanadhani ni siasa
muhimu zinazotakiwa, wapo na sisi,” .
“Nahitaji
majimbo yote ya Kigoma kuchukuliwa na ACT bila kukosa hata moja na hili
hata Serukamba (Mbunge wa Kigoma Mjini-CCM) analijua. Mwanasiasa
anayetaka kuwa mbunge Kigoma lazima aje ACT,” alisema Zitto ambaye pia alirejea kauli yake kuwa atagombea ubunge katika jimbo jingine lakini siyo Kigoma Kaskazini.
Kauli hiyo ya Zitto inawagusa wabunge wa sasa wa majimbo ya Kigoma ambao ni; Felix Mkosamali (Muhambwe), Moses Machali (Kasulu Mjini), Agripina Buyogela (Kasulu Vijijini) na David Kafulila (Kigoma Kusini), wote wa NCCR-Mageuzi na Peter Serukamba (Kigoma Mjini, Christopher Chiza (Buyungu) na Albert Obama (Manyovu) wa CCM.
MWANANCHI
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa
amesema anashindwa kujitokeza kuzungumzia au kufanya mambo
yanayohusiana na urais kwa kuwa Kamati ya Maadili ya CCM inamfuatilia
kwa karibu.
Alisema hayo jana alipoulizwa kuhusu kauli ya Rais Jakaya Kikwete wiki iliyopita akiwa Marekani ambako alielezea mafanikio na changamoto alizokumbana nazo wakati wa uongozi wake wa miaka 10.
Kikwete alisema:
“Wakati unaingia Ikulu unakuwa na shauku kubwa pamoja na furaha ya
ushindi, lakini hakika urais ni kadhia kubwa. Ukipata fursa ya kuwa rais
kwa awamu mbili kama mimi nadhani zinatosha kabisa. Nimefanya mengi kwa
nchi yangu atakayekuja ataendeleza nilipoishia.”
Kauli ya Lowassa inakuja ikiwa ni siku
chache baada ya makada wengine wanaotajwa kuwania urais kupitia CCM
kueleza maoni yao juu ya kauli hiyo ya Rais.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba
ameshalieleza gazeti hili kuwa kauli hiyo inampa hamasa kwa nia yake ya
kutaka kuwania urais na kwamba alitangaza nia hiyo huku akifahamu kwa
asilimia 100 uzito wa jambo hilo akisema kufahamu changamoto hizo ndiyo
moja ya vitu vilivyomsukuma kuchukua uamuzi huo.
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye alisema:
“Kama mtu ameamua kuwania nafasi hiyo ina maana anafahamu anachokitaka.
Tunajua ziko changamoto na namna ya kukabiliana nazo, kwa hiyo hakuna
sababu ya kuwa na wasiwasi.”
Mbunge wa Nzega, Dk Hamis Kigwangalla alisema:
“Kauli kama hiyo haiwezi kumvunja mtu moyo, ari itabaki palepale tu kwa
aliyetangaza nia. Aliyetangaza nia anataka kutoa utumishi wake kwa nchi
yake kama mimi.”
Lowassa hajatangaza wazi nia hiyo zaidi
ya kusema ameshawishika kuwania urais baada ya hivi karibuni, makundi
mbalimbali kufika nyumbani kwake mjini Dodoma kumshawishi achukue fomu
kuwania nafasi hiyo.
Miongoni mwa makundi yaliyojitokeza na
kumshawishi pamoja na kumchangia fedha za kuchukua fomu ya kugombea
urais ndani ya CCM ni pamoja na masheikh kutoka wilayani Bagamoyo,
wachungaji wa makanisa ya Kipentekoste, wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja
na madereva bodaboda.
Akizungumza jana wakati wa kuaga mwili wa Mkurugenzi wa zamani wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk Mohamed Mhita nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es Salaam, Lowassa alisema: “Muda mwafaka ukifika nitatangaza nia na kuweka mikakati yangu wazi ili wananchi waijue.
Kwa sasa siwezi kusema chochote kwa
sababu ninatazamwa sana na chama. Ninachoweza kusema, siku
nitakayotangaza nia, nitaeleza ni nini nitafanya kukabiliana na
changamoto zote zilizopo Ikulu.
MWANANCHI
Upungufu wa chakula kwa baadhi ya mikoa
nchini umeendelea kusababisha ongezeko la mfumuko wa bei wa Taifa
kutoka asilimia 4.2 hadi asilimia 4.2 ndani ya mwezi mmoja.
Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraimu Kwesigabo, aliwaambia waandishi wa habari leo kuwa, kutokana na upungufu huo bei za bidhaa za vyakula zimeongezeka.
“Mfumuko
wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapimwa kwa kiwango cha badiliko
la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi,”Kwesigabo.
Aliongeza: “Hivyo kutokana na ongezeko la bei za bidhaa hizo pamoja na huduma zote kwa kaya zimesababisha mfumuko wa bei wa taifa,” Kwesigabo.
Aliendelea kueleza kuwa, kasi ya
upandaji wa bei za bidhaa hizo zimesababisha mfumuko wa bei wa Taifa kwa
mwezi iliyopita kuongezeka hadi ukufikia asilimia 4.3 kutoka asilimia
4.2 ya mwezi Februari mwaka huu.
Kwesigabo alisema, ongezeko la mfumuko
wa bei kwa mwezi Machi umesababishwa hasa na kuongezeka bei za bidhaa za
vyakula kwa kipindi kilichoishia Machi mwaka huu tofauti na ilivyokuwa
kwa Machi mwaka jana.
Alizitaja bidhaa hizo kuwa ni pamoja na mchele, unga wa muhogo, nyama, samaki, maharage, choroko na sukari.
Alisema kutokana na hali hiyo wananchi
wataendelea kushuhudia bei za vyakula zikiendelea kupanda na kwamba bei
waliyokuwa wakinunua bidhaa za vyakula hapo awali itabadilika.
Akizungumzia thamani ya shilingi ya
Tanzania kwa mwezi uliopita ikilinganishwa na mwezi Septemba, 2010
alisema, uwezo wa Sh 100 katika kununua bidhaa na huduma umefikia Sh 64
na senti 15 mwezi Machi mwaka huu kutoka Septemba, 2010.
“…ikilinganishwa na Sh 64 na senti 59 ilivyokuwa Februari mwaka huu,”Kwesigabo.
HABARILEO
Mzee mwenye umri wa miaka 68, Celestine Mushi,
mkazi wa kata ya Motamburu wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, ameuawa
na wananchi wanaotajwa kukasirishwa na kitendo chake cha kupeleka
waganga wa jadi kijijini kwa lengo la kuifanyia zindiko nyumba yake.
Mushi anadaiwa kuwatoa waganga hao wawili jijini Dar es Salaam na kuwapeleka Rombo kwa kazi hiyo maalumu.
Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Godfrey Kamwela
aliyesema mauaji hayo yalitokea juzi saa 2.30 usiku nyumbani kwa Mushi
katika kitongoji cha Mbomai Juu, wakati waganga hao wakiendelea na
zindiko lao.
Kamwela aliwataja wanaodhaniwa ni waganga wa jadi kuwa ni Ashraf Mjengwa (22) na Peter Mmaka (25), wote wakazi wa Magomeni, Dar es Salaam.
Alisema waganga hao walifika nyumbani
kwa Mushi juzi saa 10 jioni, na ilipofika saa 11 walianza shughuli ya
zindiko na walipomaliza, Mushi alitaka kuwapeleka katika nyumba ya mkwe
wake aitwaye Priscila Hilment, ili nayo ifanyiwe zindiko.
Kamwela alisema kitendo hicho
kilikataliwa na mama mkwe, ambaye alipiga kelele kuomba msaada kwa
wananchi ili wawaondoe waganga hao, ambapo wananchi walifika na
kuwashambulia waganga hao.
Alisema kutokana na tafrani hiyo, raia
mmoja alitoa taarifa katika kituo cha polisi, ambapo polisi walifika
eneo la tukio na kufanikiwa kumwokoa mganga mmoja, Mjengwa, ambapo
mwenzake alikimbia na kutokomea kusikojulikana.
Kamwela alisema ilipofika saa 2 usiku,
kundi la wananchi wasiojulikana idadi yake walirudi nyumbani kwa mzee
huyo na kuanza kumpiga kwa fimbo kichwani na sehemu mbalimbali za mwili
wake, na kisha kuondoka na kumwacha akivuja damu nyingi.
Alisema kutokana na damu kuendelea
kuvuja, mtoto wa mzee huyo alimchukua baba yake na kumpeleka katika
kituo cha afya cha Tarakea, ambapo alifariki dunia kabla ya kupatiwa
matibabu na Jeshi la Polisi limeanza msako wa kuwatafuta wahusika.
HABARILEO
Wanawake wenye umri mkubwa wametakiwa
kuacha kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na vijana wenye umri mdogo,
kwani jambo hilo linawapunguzia heshima katika jamii.
Ushauri huo ulitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Halima Kihemba wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Afya Duniani yaliyofanyika eneo la Kituo cha Afya Mlandizi, wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Kihemba, ambaye kitaaluma ni
mwanahabari, alisema kuna ripoti za kipolisi mkoani Pwani zinazoeleza
kuna kinamama ambao tayari wamevuka umri wa miaka 60 wana uhusiano wa
kingono na vijana wenye umri mdogo, jambo linalowapunguzia heshima
katika jamii.
“Kuna
taarifa kuwa miongoni mwenu kuna kina mama wana tabia mbaya ya kuwa na
wapenzi ambao ni vijana wadogo sana kiumri. Kweli si kweli? Aliuliza mkuu huyo wa wilaya na wazee hao ambao kwa idadi walikaribia 300, wakaitikia ‘Kweliiiii’.
Akizungumzia ukubwa wa tatizo hilo mkoani humo ambapo alisema “Halijawa
tatizo kubwa sana, lakini kuna wachache walio na tabia hizo mbaya, ndio
maana tunaanza kulidhibiti ili lisisambae kwa kasi maeneo mengine.”
Alisema tatizo hilo kwa ukubwa lipo miongoni mwa wanaume ambao wamekuwa
wakijihusisha na ndoa za utotoni kwa muda mrefu, huku likilazimisha
wanafunzi wa kike kukatisha masomo yao kuolewa.
Uchunguzi uliofanywa miongoni mwa wazee
ambao walikuwa wanapata huduma ya bure ya kupima afya zao kwa msaada wa
shirika lisilo la kiserikali la The Good Samaritan Social Services umethibitisha ubakaji na ndoa za utotoni ni matatizo makubwa maeneo ya Mlandizi na viunga vyake.
Mkurugenzi wa Shirika hilo, Elisha Mwamkinga alisema shirika lake linajitahidi kuwaelimisha wazee kuishi kwa heshima katika jamii na kuepuka mambo ya aibu miongoni mwao.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitiaKama kawaida tangakumekuchablog inakupatia uchambuzi wa magazeti na kujua kwa kina yote yaliyoripotiwa na vyombo vya habari ni hapa hapa www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment