MWENYEKITI JUMUIYA YA WAFABIASHARA AACHIWA KWA DHAMANA
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania, Johnson Minja, (mwenye koti la
kahawia), akisindikizwa na mawakili na wafanyabiashara
wenzake.MWENYEKITI huyo wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini,
ameachiwa kwa dhamana leo jijini Dodoma baada ya kushikiliwa kwa siku
sita kufuatia kuondolewa dhamana ya awali kwa madai ya kukiuka masharti
ya dhamana.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa
Dodoma ikiwa ni siku moja baada ya suala lake kuibuliwa bungeni mjini
Dodoma kwa baadhi ya wabunge kuitaka serikali kukaa na kuangalia namna
ya kuweza kumaliza mgogoro uliopo kwa kupatiwa dhamana kwa mwenyekiti
huyo.
Kushikiliwa kwa Minja kumesababisha kuwepo migomo ya wafanyabiashara wenye maduka
katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Tanga waliokuwa wamefunga maduka yao
kushinikiza kuachiwa kwa mwenyekiti wao huyo.
No comments:
Post a Comment