Thursday, April 9, 2015

REKODI NYENGINE HII HAPA

Rekodi nyingine kwa Cristiano Ronaldo hii hapa mtu wangu…

ronaldo3Usiku wa jana jumatato Cristiano Ronaldo ambaye kwa sasa ndiye mchezaji bora wa dunia ameandika historia nyingine ndani ya klabu yake ya Real Madrid.
Akiwa tayari amecheza mechi 288 tangu ajiunge na klabu hiyo, Ronaldo ambaye ni raia wa Ureno aliweza kuisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 huku akifunga bao moja ambalo limehitimisha idadi ya mabao 300 ambayo tayari amefunga tangu ajiunge na Real.
ronaldo
Ronaldo alifunga bao lake la 300 wakati Real Madrid ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Rayo Valcono iliyokuwa nyumbani katika uwanja wake wa Teresa Rivero katika mechi ya La Liga.
ronaldo2
Bao la pili la Real lilifungwa na James Rodriguez.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment