Senator wa Nairobi Mike SONKO leo kwenye HEADLINES nyingi za Kenya..
Senator wa Nairobi Mike Sonko huenda
watu wengi wakamfahamu zaidi yeye kuliko viongozi wengine walio kwenye
ngazi za juu Kenya, mavazi yake.. maisha yake.. viko tofauti sana na
jinsi viongozi wengine walivyo.
Hii ni story kubwa ambayo nimekutana
nayo leo imeandikwa zaidi kwenye mitandao ya Kenya, inahusu Senator huyo
kujiuzulu kutokana na kutajwa kwenye Ripoti ya kashfa ya Rushwa, ambapo
jana March 31 2015 Taasisi ya Kupambana na Rushwa na Ufisadi Kenya
ilitaja majina zaidi ya 100 ya watu ambao wako kwenye kashfa za rushwa.
Baada ya jina lake kutajwa alikuwa
kiongozi wa kwanza kutangaza kujiuzulu huku akisema kwamba anahitaji
kazi ya uchunguzi juu ya kashfa hizo ifanyike kwa uhuru kabisa huku yeye
akiwa nje ya ofisi yake.
Sonko amesema anatii sheria za nchi yake, anamheshimu Rais Kenyatta kwa hiyo anachokifanya ni kupisha uchunguzi kama ambavyo Rais Kenyatta ameagiza kwamba kila aliyetajwa anatakiwa aachie ofisi ili ufanyike uchunguzi juu ya tuhuma hizo.
Headlines zenye story za Senator huyu ni
nyingi, lakini moja ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara ni ishu ya
wapi anatoa pesa za kutolea huduma kama za magari ya Ambulance,
Breakdown, Zimamoto, bure kabisa kwa watu wake wa Nairobi?
Story ambayo imeripotiwa na Radio Jambo Kenya..
No comments:
Post a Comment