Wednesday, April 1, 2015

VIMBWANGA VYA WALIMWENGU

Baba mdogo wa marehemu apigwa, kisa ni kuzuia mwili wa Marehemu usiingie kwenye nyumba yake

rip_logo_farbig_rotMzee mmoja amepigwa huko Kimara Dar, baada ya kijana aliyekuwa anaishi nae ambae ni mtoto wa kaka yake alipata ajali na kufariki, wakati wa mazishi mzee huyo akakataa maiti isipelekwe nyumbani kwake kwa madai kuwa anamdai marehemu.
Kijana ambae ni rafiki wa marehemu amesema Mzee huyo alikataa maiti isiingie nyumbani kwake kwa madai kuwa ni uchuro na anamdai marehemu shilingi laki tatu, wakavunja geti na kuingia ndani lakini bado aliwakatalia, wakaamua kwenda kwenye uwanja wa mpira ili watu wapate nafasi ya kuaga mwili wa Marehemu.
Mwenyekiti wa eneo hilo alifika akamshauri mzee huyo aende uwanjani kuaga, alipofika vijana hao walianza kumpiga na kumzuia kusafiri na mwili wa marehemu kwenda Moshi kwa ajili ya mazishi.
Mzee huyo alipoulizwa sababu ya kukataa maiti isiingie ndani kwake alikataa kuzungumza.

No comments:

Post a Comment