Kukiwa na usafiri kama huu Dar es salaam utakwenda Town na gari lako kweli?
 Wakati
 Dar es salaam Tanzania bado inasubiri kuanza kufanya kazi kwa mabasi 
yaendayo haraka, sasa hivi nakupeleka moja kwa moja kwenye jiji la 
Barcelona Spain, jiji ambalo mpaka mwaka 2011 lilikua na watu zaidi ya 
milioni moja na laki sita ndani yake na sasa wanasema kuna zaidi ya watu
 milioni 5 ambapo ni jiji la pili kwa ukubwa kwenye nchi ya Hispania.
Wakati
 Dar es salaam Tanzania bado inasubiri kuanza kufanya kazi kwa mabasi 
yaendayo haraka, sasa hivi nakupeleka moja kwa moja kwenye jiji la 
Barcelona Spain, jiji ambalo mpaka mwaka 2011 lilikua na watu zaidi ya 
milioni moja na laki sita ndani yake na sasa wanasema kuna zaidi ya watu
 milioni 5 ambapo ni jiji la pili kwa ukubwa kwenye nchi ya Hispania. Unaambiwa
 usafiri huu wa Tram ulianza kufanya kazi kwenye mji wa Barcelona toka 
mwaka 1872 lakini barabara zilizokua zikitumika na Tram za zamani 
zilifungwa ilipofika mwaka 1971 na nafasi yake ikachukuliwa na Mabasi 
pamoja na Treni za chini ya ardhi.
Unaambiwa

Hizi zilitumika Hispania kwenye miaka ya 1960 baada ya kuchukuliwa baada ya kutumika Washington Marekani
Kwenye hii picha ya juu na ya chini ni 
muonekano wa Tram za mwanzoni kabisa wakati Barcelona imeanza kutumia 
aina hii ya usafiri.
Baada ya mapito yote hayo sasa hivi mji wa 
Barcelona unatumia Tram za kisasa zinazopita kwenye njia yake ya reli 
kama kawaida na wamezitengenezea sehemu yake iliyo na mvuto zaidi kama 
unavyoona kwenye picha hapa chini na barabara hiyo usafiri mwingine 
wowote hauruhusiwi kupita.

Usafiri mwingine unaotumika sana Barcelona 
ni usafiri wa Treni za chini kwa chini, yani zinapita chini ya ardhi na 
kusafirisha watu kwenda sehemu mbalimbali ndani ya mji, ni usafiri 
maarufu kwa jina la Metro.
Mfumo wa nauli kwenye Treni hizi za chini 
maarufu kama Metro unatumia kadi kama za ATM ambazo unaweza kulipia 
safari nyingi na ukifika kwenye mlango wa kuingilia kama huu hapa chini 
unaipitisha ile kazi kisha mlango unakuruhusu kupita kuingia kwenye 
kituo na kupanda Treni ya safari yako.

Hii
 ni sehemu ya kutazama vituo na maelekezo ya unakokwenda, mchoro huu upo
 kwenye vituo vya Treni hizi pamoja na ndani ya Treni zenyewe, ukitaka 
kujua unaposhukia kuna taa huwa inawaka kwenye viduara vyenye majina ya 
vituo so inakujulisha tuko kituo gani kwa sasa na kituo kinachofata
Kumbuka hii ni chini ya ardhi, Metro huwa 
zinatumiwa na watu wengi sababu hakuna foleni na sasa usalama upo japo 
kuna wale Wanawake wa Romania wanaotajwa sana kuibia watu mifukoni ndani
 ya hizi Treni, ukiachia hiyo huu ni usafiri salama wa kuutumia na hamna
 wezi wa kukaba hata iwe usiku wa saa ngapi.

No comments:
Post a Comment