Wakenya walivyohitimisha maombolezo ya watu waliofariki Garissa
Jana April 7 ilikuwa siku ya tatu ya maombolezo baada ya shambulio la kigaidi Chuo Kikuu cha Garissa Kenya, watu waliweka misalaba na mishumaa katika viwanja vya Nairobi kuwakumbuka wanafunzi 148 waliouawa katika shambulio hilo.


Zaidi ya watu 2000 walikusanyika kulaani
mashambulizi hayo huku Mahakama kuu ikitoa mwezi mmoja kwa Polisi
kuwahoji watu sita waliokamatwa mpaka sasa kwa kuhusika na tukio hilo
ambapo kati yao anatajwa kuwepo Mtanzania mmoja.
Kenya imefungia account za Benki za watu 86 ambao wanahisiwa kukisaidia Kikundi cha Al-Shaabab.







Hutopitwa na habari na niko tayari kukutumia muda na wakati wowote kupitia hapa hapa
ww.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment