Wednesday, April 8, 2015

WASUTANA MBELE YA KADMNASI, KWA UMBEA

 Wanawake wasutana yani.. Kisa ni maneno ya uongo yaliyoleta ugomvi

 lci-radio-on-air-2736789ywgsi_1713Wanawake wamekutana.. wote wanamlalamika msichana mmoja kwamba ana tabia ya umbea na kuchonganisha wenzake kusambaza maneno ya uongo ikiwemo kuwasingizia watu kuwa wameathirika na VVU.. wengine wamefikia ugomvi wa kupigana kabisa.
Msichana aliyempiga mwenzake kutokana na maneno ya uchonganishi, amesema msichana huyo amekuwa akimsababishia matatizo kwa kumchonganisha na watu, pamoja na mume wake.
Siku ya tukio akatokea msichana mwingine ambaye alikuwa anajua kwamba wanawake hao wamepanga kumsuta, akamwambia akimbie.. wanawake hao walikasirika kumkosa mwanamke huyo, wakaamua kumgeuzia kibao kumsuta msichana huyo aliyemfanya akimbie.
msc
Msichana aliyepigwa kutokana na maneno ya uchonganishi yaliyoenezwa na msichana huyo

No comments:

Post a Comment