Sunday, August 16, 2015

AYUPWA MIAKA 30 JELA KWA KUMUAMBUKIZA UKIMWI BINTI 9

Miaka 130 jela kumuambukiza mtoto Ukimwi

Mahakama moja nchini Kenya imetoa kifungo cha miaka 130 jela mtu mmoja  kwa kumbaka na kumuambukiza mtoto mwenye umri wa miaka 9 ukimwi.
Katika kikao hicho Mahakama kuu ya Kenya mjini Kisumu imempata na hatia  John Okewo mwenye umri wa miaka 25 na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 9 ambaye jina lake limebanwa.
Hakimu mwandamizi Aswani Opande alimpata na hatia  Okewo kwa kumabaka mtoto huyo na akamhukumu kifungo cha miaka 100 jela.
Katika shtaka la pili hakimu huyo mkuu wa eneo la Tamu lililoko Muhoroni alimhukumu mstakiwa kifungo cha miaka mingine 30 kwa kumuambukiza msichana huyo mwenye umri wa miaka 9 ugonjwa wa Ukimwi.

Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 9 anaendelea na matibabu maalum ya wanawake baada ya kujeruhiwa katika tukio hilo.
Alipopewa fursa ajitetee, mshtakiwa aliomba asamehewe kwani ni ''shetani aliyemdanganya'' kutenda maovu hayo.
Hata hivyo Hakimu akakataa kabisa kumuonea huruma na akamhukumu kifungo cha miaka 130 jela ili iwe funzo kwake na kwa wengine wenye mawazo potofu kama yake.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapatangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment