Wednesday, August 12, 2015

BBC MEDIA ACTION NA MCT WAWANOA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA KASKAZINI MJINI MOSHI

  Washiriki wa mafunzo kutoka vyombo mbalimbali  vya habari kanda ya Kaskazini, Arusha, Moshi, Manyara na Tanga  wakimsikiliza mwandishi mwandamizi, Atilio Tigalile juu ya kuandika habari za uchaguzi mkuu mwaka huu kwa usahihi bila kushabikia vyama mafunzo ambayo yameandaliwa na Baraza la Habari la Taifa (MCT) na BBC Media Action na kufanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa muda wa siku tano.



 Mwandishi wa siku nyingi ambaye pia ni mkufunzi, Atilio Tigalile, akiwaonyesha  Gazeti la Mwananchi waandishi wa habari kanda ya Kaskazini , Arusha, Moshi, Manyara na Tanga namna ambavyo habari zake haziegemei upande wowote wa vyama na wagombea wakati wa mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi mafunzo ambayo yameitishwa na Baraza la Habari la Taifa (MCT) na BBC Media Action na kufanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa siku tano.

Mkurugenzi wa blog hii ni mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo yanayoendelea mjini Moshi kwa siku tano mfululizo ikiwa ni kujengewa uwezo wa kuweza kuripoti uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika October mwaka huu.
Mafunzo hayo ambayo yananolewa na waandishi nguli akiwemo Atolio Tigalile ambaye amewahi kufanyia kazi mashirika makubwa ya habari yakiwemo, Dochwelee, Channel Afrika ya Afrika Kusini na Voice of Amerika.
Wakati wa mafunzo hayo waandishi hao wameweza kushiriki mafunzo (Field work) na kuweza kuhitimu kwa uzuri mafunzo jambo ambalo wakufunzi walilifurahia.

No comments:

Post a Comment