Depay wa Man United aomba namba maalum.
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Manchester United Memphis Depay amemuomba kocha wa timu hiyo kumkabidhi jezi namba 7 ambayo kwa sasa haina mtu kwani anaamini kuwa ana kila sifa za kuitendea haki jezi hiyo .
Depay amemuomba kocha Louis Van Gaal kumkabidhi jezi hiyo kwa sababu kwa sasa haina mtu baada ya kuuzwa kwa winga Angel Di Maria ambaye amevaa jezi hiyo kwa muda wa msimu mzima kabla ya kuondoka na kuhamia Paris St Germain.
Jezi namba 7 kwenye klabu ya Manchester United ina historia ya kipekee ambapo imezoeleka kuwa wachezaji wanaovaa jezi hiyo mara nyingi huwa wachezaji mahiri na wenye uwezo mkubwa ambao siku zote wamekuwa wkaiweka historia kwenye klabu hiyo .
Jezi hii imewahi kuvaliwa na wachezaji kama George Best , Bryan Robson , Eric Cantona , David Beckham , Cristiano Ronaldo , Michael Owen na Antonio Valencia .
Memphis Depay hadi sasa amekuwa akivaa jezi namba 9 kwenye michezo ya Pre Season na kocha wake Louis Van Gaal ameelezwa kufurahishwa na kitendo cha mchezaji huyo kuomba jezi hiyo kwani kinaashiria kujiamini kwake jambo ambalo linaweza kumsaidia kama mchezaji anayechipukia .
Namba za wachezaji zitafahamika rasmi hapo kesho (Ijumaa) katika muda ambao umewekwa kama muda wa mwisho wa timu zote kuwasilisha namba rasmi ambazo wachezaji husika watakuwa wanazivaa kwa ajili ya msimu wa mwaka 2015/2016.
No comments:
Post a Comment