Pichaz 18 za Makocha wa zamani Ligi Kuu Uingereza ambao walikuwa Wachezaji pia…
Katika hali ya kawaida imezoeleka kuwa makocha wa timu za soka mara nyingi huwa wamewahi kucheza soka katika kiwango cha juu au walau kiwango fulani ambacho kinawaruhusu kuwa na uelewa mpana wa mchezo huu.
Makocha wa timu za ligi kuu ya England wengi wao wamewahi kucheza soka katika ngazi ya juu wakitumikia klabu kubwa na zile za madaraja ya kati na hata timu za Taifa huku wakishiriki Michuano mikubwa kama Kombe la Dunia , Ligi Kuu ya England, michuano ya Kombe la Ulaya na mingine mingi.
Katika makocha wanaofundisha timu za ligi ya England kocha wa Aston Villa, Tim Sherwood amewahi kutwaa Ligi hiyo akiwa mchezaji wa klabu ya Blackburn Rovers katika msimu wa mwaka 1994/95.
Kocha wa Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino aliwahi
kuwa sehemu ya timu ya taifa ya Argentina akishiriki kwenye Kombe la
Dunia ambapo alikuwa sehemu ya idara ya kiungo kwenye timu hiyo.
Kocha wa Crystal Palace, Alan Pardew aliwahi kuichezea timu hiyo na aliwahi kuifungia bao muhimu kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Liverpool kabla ya kufika hatua ya fainali ambapo walifungwa na Manchester United.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment