Tanga,UCHAGUZI
kumpata Diwani kata ya Kiomoni halmashauri ya jiji la Tanga, umeingia dosari
baada ya wagombea watano kupinga ushindi wa Salim Hamza alieibuka kidedea na
kuutaka Uongozi wa CCM kata na Wilaya kuurudia.
Wakizungumza na waandishi wa habari
jana mara baada ya kutolewa matokeo hayo, wagombea hao walisema haiwezekani
baadhi ya vituo kukosa hata kura moja.
Walisema katika kituo cha Mbuyuni na
Mabavu mgombea, Shunda Rashid hakupata kura hata moja ilhali yeye na mke wake
wamepiga kura lakini matokeo yalionyesha amepata kura sifuri.
“Mimi na mke wangu pamoja na watoto
na wazazi wangu tulipiga kura kituo cha Mbuyuni ----eti matokeo yanatangazwa
sikupata kura hata moja hii jamani si ni wizi wa kimachomacho” alisema na
kuongeza
“Basi wizi huo ungefanyika kisayansi
kura yangu na mke wangu angalau wangeiweka na watu kuamini-----sasa kupata kura
ziro inamaanisha hata mimi mwenyewe sijajipigia kura jambo ambalo haliwezekani”
alisema Shunda
Kwa upande wake mmoja wa mgombea wa
kata hiyo, S . M Kakuru, alisema wakati
wa uhesabuji wa kura alidai kuwa alikuwa anaongoza na kushangazwa matokeo
kubadilika.
Alisema katika vituo vya Muheza,
Pande na Kiomoni alikuwa akiongoza hivyo kushangazwa na utoaji wa maotokeo na
kuadhimia kuweka pingamizi mahakamani kulalamikia mchakato mzima wa
utangazaji matokeo.
“Vituo vingi niliambiwa nimeshinda
na kuwa na matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi-=----haya matokeo ya
kutangazwa usiku wa saa tisa na kutangazwa mshindi limetutia wasiwasi” alisema
Kakuru
Wagombea hao wa nafasi ya Udiwani
kata ya Kiomoni walikuwa ni, Kauli Makame, Shunda Rashid, Kakuru S, M, Mahendra
Mulhand Shah, Abdalla Shaban na Salim Hamza ambaye ameibuka kidedea.
Katibu kata wa kata ya Kiomoni halmashauri ya jiji la
Tanga, Ramadhani Ally, akitoa ufafanuzi wa mchakato wa uchaguzi ulivyoenda na
matokeo kutangazwa jambo ambalo wananchi
walipingana nae na kuzusha tafrani na kupelekea kuondoshwa katika eneo la tukio
ili kuleta hali ya usalama.
Wakazi wa kijiji cha Kiomoni halmashauri ya jiji la Tanga, wakimoundoa Katibu kata wa kata hiyo , Ramadhani Ally baada ya kutoa ufafanuzi wa mchakato wa matokeo katika vituo na kumtuhumu jambo ambalo lilizusha tafrani na kuelezwa kuwa yeye hana mamlaka ya kutoa ufafanuzi wakati mshindi ameshatangazwa na kupatikana.
No comments:
Post a Comment