Mchezo wa ng'ombe wawaua watu 7 Uhispania
Ng'ombe
wanaotumiwa katika mchezo wa Matador wamewaua watu saba katika sherehe
nchini Uhispania tangu mwanzo wa mwezi Julai huku wanne wakiuawa wikendi
iliopita.
Vifo hivyo vilitokea wakati wa kufukuzana na ng'ombe hao katika barabara na sio ndani ya ukumbi wa mchezo kama ilivyozoeleka kama kule visiwani Zanzibar ambako inasemekena kuwa ndio chimbuko la mchezo wa ng'ombe ulikoanzia.Mchezo huo wa ng'ombe ambao unasemekana kuwa ndio hatari umekuwa kivutio hasa wachezaji wake wanavyoujua kuucheza ila kwa miaka ya hivi karibuni mchezo huo umefifia.
Inadaiwa kuwa kwa sasa mchezo wa ng;ombe unabaki simulizi tu ila kwa wenzao wa Ulaya ni mmoja wa mchezo unaopendwa sana badala ya mpira wa miguu na kikapu
Miongoni mwa waliouawa ni diwani mmoja mwenye umri wa miaka 36 aliyeuawa katika mji wa Penafiel,mji ulio karibu na ule wa Valladolid kaskazini mwa Madrid.
Vifo vyengine vilitokea wakati wa sherehe za ngombe katika majimbo ya Valencia,Murcia,Toledo,Castellon na Alicante hivi karibuni.
Kwa habari matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog.
No comments:
Post a Comment