Monday, August 3, 2015

MTOTO WA MIAKA 15 ASOMEA PHD

Huyu ndie msichana ambae anasoma PhD India na umri wake ni miaka 15 tu…!!

India
Sushma Verma na wazazi wake siku ya Graduation yake akimaliza Masters.
Kwa hesabu ya kawaida tu, mtoto anaanza Shule ya akiwa na miaka sita, au saba hivi… alafu mpaka kumaliza anakuwa na kama miaka 14, sasa kuna mtu kwenye umri huo alikuwa kamaliza high school na alikuwa Chuo tayari anamaliza  degree!!
india-child-prodigy
Anaitwa  Sushma Verma ni msichana ambaye umri wake ni miaka 15, aligraduate Degree ya Microbiology Chuo cha Lucknow kilichopo India na kajiunga Babasaheb Bhimrao Ambedkar University (BBAU) kwa ajili ya kusomea Masters, kamaliza mwezi June 2015 na anaendelea kujipanga ili kuendelea na masomo ya PhD.
India II
Hii ilikuwa wakati Sushma Verma anasoma Masters, alikuwa na miaka 13 tu.. kuna wakati baba yake ilibidi atumie baiskeli kumsindikiza mwanae shule.
Sushma amewashangaza wengi lakini ndio hivyo, ana uwezo mkubwa sana darasani kitu ambacho Mkuu wa Chuo hicho amemuahidi kumpa ofa ya kulipiwa ada pamoja na Hostel bure akianza PhD ya environmental microbiology >>> “Lazima tumpe moyo kwa kipaji chake, tutamsajili na kumpatia Hostel na scholarship pia” >>> Prof. R C Sobti, Makamu Mkuu wa Chuo Babasaheb Bhimrao Ambedkar University.
Ungana nami kwa matukio , habari na michezo hapa hapa tangakumekuchablog

2 comments: