Monday, August 10, 2015

MWANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO APIGWA HADI KUFA

Ripota wa Spoti apigwa na mashabiki hadi kufa

Mwandishi wa habari za michezo  amepigwa hadi kufa na mashabiki ..
Rasim Aliyev raia wa Azerbaijan alimkashifu mchezaji nyota wa klabu ya Gabala ;Javid Huseynov, katika mtandao wa kijamii wa facebook.
Aliyev aliandika '' Huseynov na timu ya kandanda ya Gabala wanapaswa kupigwa marufuku ya kushiriki mashindano yeyote ya bara Ulaya kwa kupeperusha bendera ya Uturuki

Tukio hilo lilitokea baada ya mechi baina ya ya mchujo ya ligi kuu ya Europa mnamo Agosti tarehe 6.
.
Dadake aliwaambia waandishi wa habari kuwa mtu mmoja alimpigia simu na kutishia maisha yake.

Inadaiwa kuwa Aliyev alikutana na mtu aliyedai kuwa binamu ya mshambulizi huyo akikusudia kuomba msamaha kwa maandishi yake.
.
Yamkini mwandishi huyo alikuwa amekubali kukutana na mtu huyo kwa nia ya kwenda kunywa chai naye kama ishara ya mapatano na uwiano lakini alipofika sehemu waliokuwa wameahidi kukutana alivamiwa na kushambuliwa na takriban watu 6 waliokuwa wamemuwekea mtego.

Aliaga dunia jana alipokuwa akipatiwa matibabu katika wodi ya wagonjwa mahututi katika hospitali kuu ya Baku.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment