Kibao kilivyowageukia Polisi waliovamia na kuwakamata wapenzi Hotelini India…
Polisi waliendesha msako kwenye Hoteli
mbalimbali India kama wiki moja hivi iliyopita, kisa cha kuendesha msako
huo walidai kwamba wenyeji wa eneo la Mumbai walilalamika kwamba kuna
mambo maovu yanafanyika kwenye maeneo yao, Polisi wakaona waingie mtaa
kwa mtaa kumalizana na wanaofanya hayo mambo !!
Wapendanao zaidi ya 20 walikamatwa
katika msako huo, lakini kibao kikageuka baada ya Polisi kufanya msako
na kuwakamata wapendanao hao katika Mahoteli mbalimbali badala ya mtaani
!
“Nimeshindwa
hata kutoka nje ya nyumba yetu, wazazi wangu hawajaongea neno hata moja
na mimi toka kumekucha… Mimi sijiuzi, ni mtu mzima na nilitoka na
mpenzi wangu ambae natakiwa kufunga nae ndoa mwezi ujao”—mmoja wa wasichana walionaswa kwenye msako huo alilalamika.
Malalamiko yamekuwa mengi sana kwenye Mitandao ya Kijamii India baada ya hii ishu japo Kamanda wa Polisi Mumbai, Rakesh Maria amepinga msako huo kufanyika kwenye Mahoteli >>> “Kama watu wazima wawili wakiwa ndani ya chumba cha Hoteli kwa mambo yao sisi haituhusu”
Moja ya website kubwa India imelaani pia hiyo ishu na hii ni moja ya sentensi zilizokosoa kitendo hicho >>> “Hakuna Sheria inayokataza watu ambao hawajaoana kuwa kwenye chumba cha Hoteli pamoja”
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment