Salva Kiir akataa kutia sahihi mkataba
Serikali
ya Sudan Kusini imekataa kusaini mkataba uliotarajiwa kuleta amani na
kumaliza mapigano yaliyodumu nchini humo kwa zaidi ya miezi ishirini.
Hata hivyo waasi na makundi ya upinzani wamesaini kwa upande wao.Serikali hiyo ya Sudani Kusini imeomba kuongezewa siku kumi na tano zaidi kushauriana juu ya mapendekezo hayo.
Waziri wa Uingereza anayesimamia maswala ya Afrika ameitaka Serikali ya Sudan Kusini kutia sahihi mkataba huo haraka iwezekanavyo.
Amesema kuwa watu hawafai kusheherekea hadi pale rais Kiir atakapotia sahihi mkataba huo.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment