Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha elimu cha Candle Education Centre Tanga, kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu, kituo pia kinatoa kozi mbalimbali za kielimu na kiufundi ikiwemo komputer na umeme. Kituo kipo Tanga mkabala na bank ya CRDB simu 0715 772746
MWANANCHI
Mawaziri wawili wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete
wameanguka kwenye marudio ya Kura za Maoni zilizofanyika juzi, huku
matokeo ya Jimbo la Busega yakikwama baada ya Waziri wa Uvuvi na
Maendeleo ya Mifugo, Dk. Titus Kamani kumshambulia msimamizi wa Uchaguzi.
Walioanguka ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid (Rufiji) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mazingira), Dk. Binilith Mahenge (Makete), huku Dk Raphael Chegeni akiongoza kwenye Jimbo la Busega.
Dk Kamani na wafuasi
walizuia matokeo kutangazwa na kuibuka kwa vurugu zilizosababisha polisi
kuingilia kati na kukamata watu wanne walioonekana kumuunga mkono.
“Aliyeshinda
ameshinda tu hakuna namna. Kilichofanywa na Waziri Kamani kumpiga
msimamizi huyo ni mambo ya binadamu tu… lakini walioshindwa lazima
wakubali matokeo na lazima yatangazwe,” alisema Paul Mzindakaya, Mkuu wa Wilaya ya Busega.
Vurugu zilianza saa 4 asubuhi baada ya
Dk Kamani, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Simiyu, kuingilia
kati wakati Mabiya, ambaye ni katibu wa Wilaya ya Meatu, akianza
kutangaza matokeo.
Baada ya Polisi waliokuwa na silaha
kuimarisha ulinzi, Mabiya alisimama kutangaza matokeo lakini akakatishwa
baada ya kurukiwa na watu walioonekana kumuunga mkono Waziri Kamani na kupigwa makonde mbele ya Polisi na Mzindakaya.
Kipigo hicho kilimfanya Mabiya akimbilie ndani ya ofisi za chama hicho na kuacha askari wa Kikosi cha FFU wakitumia nguvu kudhibiti watu hao.
Wakati wote wa vurugu hizo, Dk. Chegeni
alikuwa amesimama pembeni mwa ofisi za chama hicho akishuhudia matukio
hayo, lakini baadaye akaondoka akiwa amepanda gari lake huku
akishangiliwa.
Baada ya polisi kufanikiwa kutuliza
ghasia, Mabiya alisimama tena kutangaza matokeo hayo, lakini Dk Kamani
alimfuata na kumshambulia kwa makonde, kukazuka tafrani kubwa zaidi.
MWANANCHI
Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), limemwonya Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika
kutolihusisha na siasa, huku likikana kuwanyang’anya kadi za kupigia
kura maofisa wake ili kufanya hujuma katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Nae Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu
amesema suala hilo linapotoshwa na kuwa ni wajibu wa viongozi wa Jeshi
hilo kuhakikisha Askari wote wanatumia fursa ya kumchagua kiongozi wao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Habari na Uhusiano kwa Umma, Kanali Ngemela Lubinga alisema Jeshi limesikitishwa na kauli ya Mnyika ya kwamba limewanyang’anya kadi za kupigia kura maofisa wake .
“Wanajeshi hawaruhusiwi kabisa kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa,”– Kanali Lubinga.
Mbunge John Mnyika
alisema CHADEMA imebaini uwapo wa mbinu za kutaka kuhujumiwa kwenye
Uchaguzi Mkuu kwani Serikali imeviagiza vyombo vya usalama, kupeleka
namba za vitambulisho vya askari wote kwa wakuu wa vitengo jambo ambalo
ni kinyume na utaratibu.
NIPASHE
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imetangaza
siku ya urejeshaji fomu za Urais na Makamu wa rais kuwa ni AlhamisI
ijayo huku ikipiga marufuku maandamano, ni watu saba tu ndio
wataruhusiwa kusindikiza Wagombea.
Urejeshaji fomu utaanza saa 1:30 asubuhi
hadi saa 10:00 jioni, huku wagombea wote wakitakiwa kufika kwenye ofisi
za Tume wakisindikizwa na watu hao na majina yao yanatakiwa
yawasilishwe Tume kabla ya Agosti 20, ili kuratibu kazi hiyo.
“Wagombea
hawaruhusiwi kuja Tume kwa maandamano, shamrashamra, nderemo wala
vifijo. Hii ni kwa sababu siku hiyo vyama vya siasa vitakavyowasilisha
fomu za kuomba uteuzi vitakuwa vingi hivyo kila chama kikija Tume kwa
maandamano na shamrashamra kunaweza kutokea uvujifu wa amani,“– Mkurugenzi wa NEC, Ramadhani Kailima.
Alisema sababu nyingine ya kuanga hivyo
ni kuwawezesha wananchi wengine kuendelea na shughuli zao pamoja na
kuimarisha amani na utulivu.
NIPASHE
Hali inazidi kuwa tete ndani ya Chama
cha CCM baada ya vigogo tisa, akiwamo Mwenyekiti wa Jumuiya ya UVCCM
Vijana Mkoa wa Kilimanjaro (UVCCM), Fredy Mushi jana kujiuzulu nyadhifa zao na kutangaza kujiunga na CHADEMA.
Wengine waliotimka ni Katibu wa Uchumi na Fedha na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa CCM, Paul Matemu, Mchumi wa UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro, Jerome Komu na Noel Nnko ambaye alikuwa Mratibu wa Kanda ya Kaskazini wa Marafiki wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, wamo pia Wafanyabiashara maarufu wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, Douglas Malamsha na Peter Kirenga.
Kujitoa kwa vigogo hao, kumefanya idadi ya makada waliokihama CCM ndani ya mwezi mmoja kufikia 21.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
amesema CCM hakishtushwi na makada na viongozi wanaoendelea kukihama
chama hicho na kujiunga na CHADEMA na kudai kuwa wanaoondoka wana sababu
zao binafsi.
Amesema hakuna kiongozi wa upinzani
ambaye hakuanzia CCM hivyo ni hali ya kawaida kwa chama kikubwa kama
hicho ambacho kina mtaji wa wanachama takribani milioni nane, makada
wake kuhama.
“Waliohama,
wanaohama na watakaohama hili siyo jambo jipya lilishatokea tangu miaka
23 iliyopita na litaendelea kwa muda mrefu hivyo siyo jambo la
kushangaza, kuna viongozi wakubwa waliondoka na wengine wakarudi, Mfano
Maalim Seif na Agustine Mrema walikuwa CCM na waliondoka”—Nape Nnauye.
Nape alikanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa, Mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli, alitangaza kuwagawia kompyuta walimu wote.
Alisema taarifa hizo ni za uzushi na
kwamba Ilani ya uchaguzi ya chama hicho ilipitishwa juzi mkoani Dodoma
na inatarajiwa kuzinduliwa Agosti 23, mwaka huu.
HABARI LEO
Jeshi la Polisi Dodoma linamshikilia mtu mmoja Mohammed Abdallah baada ya kukutwa akitoa huduma za kidaktari ambazo hana utaalamu nazo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alisema Abdallah alikamatwa Agosti 12 Wilaya ya Kongwa, akiwa tayari ametoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa zaidi ya 20.
Kamanda Misime alisema
baada ya mtuhumiwa kukamatwa katika nyumba hiyo alikopanga, alipekuliwa
na kukutwa na dawa mbalimbali zenye nembo ya Bohari ya Madawa (MSD),
mifuko tisa, sindano na baadhi ya vifaa tiba vinavyodhaniwa vilipatikana
kwa njia isiyo halali.
Baada ya kuhojiwa mtuhumiwa alikiri
kutenda kosa hilo na kuongeza kwamba hana taaluma yoyote ya utabibu na
elimu yake ni darasa la saba, Kamanda Misime alisema uchunguzi zaidi unaendelea na ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani.
UHURU
Jeshi la JWTZ limesema Askari wake watappiga Kura kwenye Vituo vya Uraiani na sio ndani ya Kambi za Jeshi.
“Wanachama hawaruhusiwi kuwa Wanachama wa Chama chochote cha Kisiasa, hawaruhusiwi kuwa mashabiki wa Chama chochote”—alisema Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ, Meja Ngomelo Lubinga huku akipinga kauli ya Mbunge John Mnyika kwamba Jeshi hilo limechukua Kadi za Kupigia Kura kwa baadhi ya Askari.
Kwa habri, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment